Maginetiti

Maginetiti ni madini yenye rangi nyeusi-kijivu yenye tabia ya sumaku. Kikemia ni oksidi ya feri (chuma) yenye valensi za 2+ na 3+. Fomula yake ni Fe3+2Fe2+O4.

Maginetiti kutoka Afrika Kusini

Inatokea mara nyingi kwa umbo la fuwele zenye urefu wa karibu sentimita 1 na kona 8. Kiwango cha feri (chuma) hufikia asilimia 72 kwa hiyo ni malighafi muhimu kwa kutengeneza chuma.

Viungo vya NjeEdit