Magnificat
Magnificat (neno la Kilatini lenye maana ya: "Inatukuza") ni jina la utenzi unaotumika sana katika liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika Masifu ya jioni. Jina hilo linatokana na neno la kwanza la wimbo huo katika tafsiri ya Kilatini.
Wimbo huo ni maarufu pia kama Wimbo wa Maria, kutokana na mtunzi wake kadiri ya Injili ya Luka 1:46-55.
Ni mmojawapo kati ya nyimbo nne zinazopatikana katika Injili hiyo.[1][2]
Humo tunasoma kwamba Bikira Maria alitoa moyoni maneno hayo ya sifa kwa Mwenyezi Mungu akiwa na mimba ndogo ya Yesu baada ya kumshangiliwa na jamaa yake Elisabeti aliyeangazwa na Roho Mtakatifu kuhusu hali yake ya ujauzito na kuhusu ukuu wa mtoto huyo hata akamuita "Mama wa Bwana wangu". Elisabeti alimpongeza Maria kwa baraka hiyo aliyoipata, kubwa kuliko ile ya wanawake wengine wote. Pia alimpa heri kwa imani yake.
Maneno yake ni haya:
Nafsi yangu yatangaza ukuu wa Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu, mwokozi wangu;
kwa sababu ameona unyonge wa mtumwa wake.
Tangu sasa vizazi vyote vitanipongeza,
Kwa sababu Mwenyezi amenitendea makuu;
jina lake takatifu,
ne rehema zake hufikia uaminifu wake
kutoka kizazi hadi kizazi.
Hufanya ushujaa kwa mkono wake:
huwatawanya wenye kiburi moyoni,
huwaangusha wenye nguvu kutoka katika viti vyao vya enzi
na kuwainua wanyonge,
huwashibisha wenye njaa vitu vyema,
na matajiri huwafukuza mikono mitupu,
Umsaidie Israeli, mtumishi wake,
akikumbuka rehema kama alivyowaahidi baba zetu.
Kwa neema ya Ibrahimu
na kizazi chake milele.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ The History and Use of Hymns and Hymn-Tunes by David R Breed 2009 ISBN 1-110-47186-6 page 17
- ↑ Favourite Hymns by Marjorie Reeves 2006 ISBN 0-8264-8097-7 page 3-5
Viungo vya nje
hariri- The Magnificat
- Exegesis and Sermon Study of Luke 1:46-55: The Magnificat, by Curtis A. Jahn Archived 18 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
- ChoralWiki: Magnificat
- "Magnificat". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- Officium pro defunctis, following the unrevised Vulgate text
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Magnificat kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |