Maisie Williams

Mwigizaji wa Uingereza

Margaret Constance "Maisie" Williams (amezaliwa Bristol, Aprili 15, 1997) ni mwigizaji wa Uingereza.

Maisie Williams
Amezaliwa15 Aprili 1997
UtaifaMtanzania
Majina mengineMargaret Constance "Maisie" Williams
Mhitimu
Kazi yakemwigizaji, mjasiriamali
Miaka ya kazi2011-hadi sasa

Williams alianza kuigiza mnamo 2011 kama Arya Stark akiwa kama mmoja ya wahusika wakuu wa tamthilia ya Game of Thrones(2011-2019). Alianza kua maarufu kupitia tamthilia hio na kuchaguliwa kuwania tuzo mbili za Emmy Award. Williams alionekana katika tamthilia zingine kama vile Doctor Who (2015) akiigiza kama Ashildr, aliigiza pia katika filamu ya Uingereza iliyoitwa Cyberbully (2015), na katika filamu ya vijana iBoy (2017). Aliigiiza pia kama muhusika mkuu katika tamthilia ya maigizo ya vichekesho iliyoitwa Two Weeks to Live (2020), na aliigiza kama Jordan katika filamu ya Pistol(2022). Williams pia aliigiza sauti ya Cammie MacCloud katika katuni ya marekani ambayo ilikua ikijulikana kama Gen:Lock (2019–2021).

Mnamo mwaka wa 2014, aliigiza kama Lydia katika filamu yake ya kwanza iliyoitwa The Falling, ambayo ilimpa umaarufu na kupata baadhi ya tuzo. Na pia aliigiza kama muhusika mkuu katika filamu kama Mary Shelley (2017), katuni ya vichekesho Early Man (2018), na filamu ya mapenzi Then Came You (2018). Mnamo mwaka 2018 alicheza kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa la filamu katika tamthilia ya Lauren Gunderson I and You kwenye ukumbi wa Hampstead huko London. Mnamo 2020 aliigiza katika filamu ya kutisha The New Mutants na The Owners.

Mnamo mwaka wa 2019, Williams kwa pamoja walitengeneza na kuzindua jukwaa la mitandao ya kijamii Daisie, programu ya mitandao ya media anuwai iliyoundwa kuwa njia mbadala ya kuwasaidia wasanii na watayarishi (haswa wale wanaojaribu kuanza) katika taaluma zao.

Maisha ya awali na Elimu

hariri

Margaret Constance Williams alizaliwa na Gary Williams na Hilary Frances , Mama yake alikua ni msimamizi wa kozi ya chuo kikuu ambaye baadaye aliacha kazi yake ili amsaidie Maisie katika kazi zake za uigizaji[1][2][3][4]. Wazazi wa Williams walitalikiana alipokuwa na umri wa miezi minne tu. Williams ndio mtoto mdogo kabsa kati ya ndugu zake wanne James, Beth na Ted, Williams alilelewa na mama yake na babake wa kambo katika nyumba yenye vyumba vitatu vya kulala katika kijiji cha Clutton, Somerset[5].

Williams amejulikana kama "Maisie" tangu umri akiwa mdogo[6], alipewa jina hilo la utani kwa sababu alikua anafanana na mhusika wa katuni ya vibonzo wa gazeti la Uingereza The Perishers.

Williams alisoma katika Shule ya Msingi ya Clutton na Shule ya Norton Hill huko jiji la Midsomer Norton. Baadaye alihamia Chuo cha Bath Danceambapo alisomea sanaa ya uigizaji, ambako alijifunza katika ukumbi wa michezo wa kuigiza, ballet, pointe, tap, street, mitindo huru, mazoezi ya viungo , kwa nia ya kuwa mchezaji wa kulipwa. Aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 kwa sababu ya kufanya vizuri katika kazi yake na kuamua kuanza kuigiza. Wakati huo alikuwa anasoma akiwa nyumbani, lakini hakufanya mitihani ya GCSEs yoyote[7][8][9].

Marejeo

hariri
  1. Hughes, Sarah (2016-04-22), "Game of Thrones' Maisie Williams: 'It's not all fun and games'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  2. Hughes, Sarah (2016-04-22), "Game of Thrones' Maisie Williams: 'It's not all fun and games'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  3. London, Lela (2019-05-05), "What happened to Arya Stark in the Game of Thrones finale - and what's west of Westeros?", The Telegraph (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0307-1235, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  4. Emma Elgee, Daniel Chipperfield (2019-04-28). "Everything we know about Game of Thrones' Bristolian Maisie Williams". Bristol Live (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.
  5. Cronin, Emily (2018-07-07), "Maisie Williams on finding her style, growing up in the spotlight... and the final series of Game of Thrones", The Telegraph (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0307-1235, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  6. Heawood, Sophie (2019-04-14), "Maisie Williams: 'I was covered in blood and gnawing on pizza'", The Observer (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0029-7712, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  7. Nicholson, Rebecca (2018-10-17), "Game of Thrones' Maisie Williams: 'I'm still petrified of my peers'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  8. "Game of Thrones star Maisie Williams was bullied after becoming famous", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2015-02-10, iliwekwa mnamo 2024-04-30
  9. Joe Utichi (2016-08-15). "Maisie Williams On 'Game Of Thrones' And The Future: "It Needs To Happen Organically"". Deadline (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-30.