Majadiliano:Abu Nuwas

Latest comment: miaka 18 iliyopita by 172.208.91.165 in topic Abu Nuwas au Abunuwasi?

Abu Nuwas au Abunuwasi?

hariri

Naona tatizo na mabadiliko Abu Nuwas > Abunuwasi.

Kwa sababu mbili: kwanza nimeshaweka viungo mbalimbali vya Abu Nuwas.

Pili - hapa tunahitaja maelewano kati ya watu wanaochangia kuhusu maswali jinsi ya kutaja vitu.

Jina la mtu huyu mshairi mwarabu ni Abu Nuwas.

Abunuwasi inaweza kuchukuliwa kwa namna mbili:

AMA (ninavyoona) ndiye huyu jamaa wa kifasihi wa "Riwaya" aliye tofauti na Abu Nuwas wa Kihistoria

AU ni jina la Kiswahili kwa ajili ya mshairi mwarabu Abu Nuwas; lakini sidhani ni hivyo.

Unaonaje? Sipendi kabisa tupate hivi "vita vya wahariri" jinsi ilivyo katika wikipedia nyingine

Pia naona Waswhili wanaweza kutumia ile "Abu" kuwa sehemu ya jina lao wakiiandika pekee; kwa mfano Sheikh Sayyid bin Omar bin Abdullah bin Abu Bakr bin Salim (1917-1988) aliyekuwa mkuu wa Chuo cha Kiislamu Zanzibar; ninavyoona jina la "Abu Bakr" hutumiwa na Waswahili Waislamu wengi bila kuibadilisha kuwa "Abubakri" au "Abubekri". Unaonaje, si kweli?? --Kipala 09:39, 6 Januari 2006 (UTC)Reply


Ndio Kipala. Asante, mwaka mpya salama kabisa. Hongera sana kwa kazi zako. Umeichangamsha kamusi elezo yetu. Sasa kwenye Abu Nuwas/Abunuwasi. Ni kweli hakuna haja ya kuingia kwenye vita wanavyofanya wengine. Nakubaliana nawe kuhusu jina lake halisi. Nadhani kuna majina ambayo yanapoingia kwenye Kiswahili yanabadilika kama vile Yesu. Jina lake hasa la kule alikotokea halitumiki. Au nabii Musa. Lakini kuna mengine yanabaki vile vile. Sasa katika vitabu kadhaa vya Kiswahili ambavyo nimewahi kuvipitia, nimeona jina lake limechukua kanuni fulani za Kiswahili (kwa mfano badala ya kuishia na "s" pekee ikaongezwa "i" kuwa Abunuwasi). Lakini hii inafanya jina hilo kuwa moja wakati ambapo katika maelezo yako ni kuwa haya ni majina mawili (sio?). Sasa tunaweza kuchukua vile Waswahili walivyotamka na kuandika jina lake au tukachukua jina lake halisi, ambapo itakuwa ni majina mawili kama ulivyoandika. Tunachoweza kufanya naona ni kuandika jina lake hasa (yaani lake na la ubini) kisha tukaeleza kuwa Waswahili wamekuwa wakimwita Abunuwasi. Unasemaje?
Asante kwa jibu la haraka. Kimsingi mimi naona Abunuwasi (jamaa wa kifasihi) wa "Riwaya" na mshairi Abu Nuwas (mtu wa kihistoria) si yeye yule.
Abu Nuwas alitoa jina lake kwa Abunuwasi (au labda zaidi: jina lake limechukuliwa) - hadithi zile za Abunuwasi zimesimuliwa kati ya Waturuki juu ya Nasreddin na kati ya Waarabu wengine juu ya Guha (ninaandaa makala nyingine kuhusu Riwaya nitakapoeleza uhusiano huo).
Lakini hadithi za Riwaya hazina uhusiano na Abu Nuwas wa kihistoria. Hapo sababu yangu ya kuwataja pekee.
 --172.208.91.165 13:05, 6 Januari 2006 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Abu Nuwas ".