Majadiliano:Athuman Kabongo
Latest comment: miaka 13 iliyopita by Muddyb Blast Producer in topic Jina la kisanii
Jina la kisanii
haririMzee Kipala, naunga mkono hoja yako. LAKINI pia sidhani kama Watanzania au watu wengi wa Afrika Mashariki tunamjua jina lake halisi bwana Dark Master. Hii ndiyo sababu watu wanakuja Wikipedia kuja kutazama albamu alizotoa, umri, na jina lake halisi ni nani. Ukiandika Athumani Kabongo bado shida kwa wale wanaomjua, Mzee wangu. Hii ndiyo sababu kwanza linaandikwa jina lake halisi halafu jina la kisanii baadaye pale mwanzoni kabisa mwa makala, mzee wangu. Sijui, lakini nikiwa kama mpenzi wa muziki basi najua jinsi tunavyopenda kuwaita wale wasanii tuwapendao kwa majina yao ya kisanii kuliko majina yao ya kuzaliwa! Wasalaam,--MwanaharakatiLonga 17:43, 5 Aprili 2011 (UTC)
- Sijui kama itakuwa tatizo? Kuhamisha makala kunaunda kigezo, maana yake ukitafuta "Dark Master" hutakosa makala utafikishwa kwa A Kabongo. Kimsingi naona afadhali kutumia majina ya kawaida; hasa wasanii ambao bado ni vijana hubadilisha majina baada ya muda, au la? Menginevyo nikichungulia "Dark Master" kwa google naona kuna matumizi mbalimbali; linganisha pia http://en.wikipedia.org/wiki/Dark_Masters , au http://en.wikipedia.org/wiki/Twilight_of_the_Dark_Master. Kuna pia vitabu au michezo. Kipala (majadiliano) 07:55, 6 Aprili 2011 (UTC)
- Haya, tuangalie!--MwanaharakatiLonga 16:20, 6 Aprili 2011 (UTC)