Majadiliano:FANI

Latest comment: miaka 17 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Si mambo mabaya sana yaliyo andikwa katika makala hii, sema mbona haijulikani kama wanatangaza kiswahili, kampuni, taasisi, chuo kikuu au kitu gani? Manake kaanza vizuri tu kama ushairi fulani hivi, kisha mwishoni akaja kuaribu pale alipoweka barua pepe. Hii inaashiria kuwa wanatangaza biashara au taasisi fulani kupitia wikipedia. Je hii ni sawa? Angalia kasoro ya makala hii:

1. Haikufuata taratibu za kamusi elezo hii kama inavyosema, kuanzia mwanzo wa makala hadi mwisho wa makala. Kasoro zake ni kuweka bold katika maandishi yote ya juu, hali ya kuwa yatakiwa kichwa cha habari tu ndio kiwe na bold.

2. Makala inaonekana kama ni tangazo la taasisi fulani hivi, japokuwa haja dhihilisha kama ni taasisi au kitu gani, sema yeye katumia mbinu kuu ya kuweka barua pepe ili uweze kujua nini kimejiri huko kwao.

Hapa si mahala pa matangazo ya biashara wala kampuni yoyote ile hivyo makala inahitaji marekebisho fulani. Sina la zaidi.--Mwanaharakati 11:44, 24 Novemba 2007 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " FANI ".