Majadiliano:Jerry Rawlings
Muhtasari
Jerry Rawlings ni rais wa zamani wa Ghana na afisa wa zamani wa kijeshi. Aliongoza nchi ya Ghana kutoka mwaka wa 1981 hadi mwaka wa 2001 na kwa muda mfupi mwaka wa 1979. Pamoja na viongozi wengine wa kijeshi, walitawala mpaka mwaka wa 1992. Baadaye, Mzee Rawlings aliunda National Democratic Congress (NDC) na aliwahi kuwa rais wa Ghana mara mbili.
Maisha ya utotoni
Mzee Rawlings alizaliwa mji wa Accra, nchi ya Gold Coast tarehe 22 mwezi wa 6 mwaka wa 1947. Wazazi wake wanaitwa Victoria Agbotui na James Ramsey John. Mama yake alitoka Gold Coast. Baba yake aliishi katika ngome ya Douglas katika Kirkcudbrightshire nchi ya Scotland. Makabila ya mama yake yalikuwa Nzema na Ewe lakini hii haikuathiri siasa zake.
Elimu na hudumu kwa jeshi
Alienda shule ya upili ya Achimota kisha alisoma Chuo cha Achimota. Alijunga na Jeshi la Anga la Ghana muda mfupi baadaye. Katika Jeshi la Anga, aliishi Takoradi, katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana, ili kuendelea na masomo. Yeye alihitimu mnamo mwezi wa kwanza mwaka 1969 na kuwa Afisa Mwanahewa. Yeye alikuwa luteni katika jeshi la anga la Ghana mwezi wa nne mwaka wa 1978.
Mzee Rawlings aliongoza vita mbili za mapinduzi katika mwaka wa 1979 dhidi ya Ignatius Kutu Acheampong na Jenerali Fred Akuffo na mwaka wa 1981 dhidi ya Rais Hilla Limann. Mzee Rawlings hakufurahishwa na serikali ya Ignatius Kutu Acheampong ambaye alipindua serikali nyingine na kuanza uongozi mwezi wa kwanza mwaka wa 1972. Rawlings hakumpenda Acheampong kwa sababu alishutumiwa kwa ufisadi na kuifanya nchi ya Ghana kutegemea mifumo ya serikali ya kabla ya ukoloni. Hii ilisababisha kuporomoka kwa uchumi na kuongezeka kwa viwango vya umaskini.
Mnamo tarehe 15 mwezi wa tano mwaka wa 1979, wiki tano kabla ya uchaguzi wa kitaifa, Rawlings na askari wengine sita walifanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Jenerali Acheampong, lakini walishindwa na alikamatwa na Jeshi la Ghana. Alihukumiwa hadharani kifo. Wakati wakingojea kuuawa kwake, Rawlings alitoroka kutoka kizuizini tarehe 4 mwezi wa sita mwaka wa 1979 na kikundi cha askari. Mnamo mwaka wa 1982 alijaribu mapinduzi mengine dhidi ya Rais Hilla Limann na akafanikiwa. Mzee Rawlings alitawala kupitia Provisional National Defence Council (PNDC) hadi mwaka wa 1992. Kisha akawania urais na akashinda.
Familia
Yeye alifunga ndoa na Nana Konadu Agyeman. Walikutana katika chuo Kikuu cha Achimota. Wana watoto wanne. Wana watoto watatu wa kike wanaitwa Ezanetor Rawlings, Yaa Asantewaa, na Amina Rawlings. Wana mtoto mmoja wa kiume anaitwa Kimith Rawlings.
Maisha ya baada ya urais
Mnamo mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2000, Mzee Rawlings alipewa tuzo ya kwanza ya Year of Volunteers 2001 Eminent Person na katibu wa Umoja wa Mataifa. Baada ya kupokea tuzo, alizungumza kuhusu kujitolea. Mnamo mwezi wa kumi mwaka wa 2010, yeye alikuwa mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika nchini Somalia. Sasa yeye hutoa hotuba katika vyuo vikuu.
Marejeleo
Start a discussion about Jerry Rawlings
Talk pages are where people discuss how to make content on Wikipedia the best that it can be. You can use this page to start a discussion with others about how to improve Jerry Rawlings.