Majadiliano:Jihadi

Latest comment: miaka 3 iliyopita by Kipala in topic Maana mbalimbali ya neno Jihad

Maana ya kijeshi ya Jihadi hariri

Mabadiliko ya mtumiaji:JJOSY2000 yameleta tokeo lisiloweza kuridhisha. Amebadilisha matini kwa kudai hakuna maana ya kijeshi ya istilahi hiyo, bila kuleta chanzo kinachothibitisha maelezo yake. Ameingiza chanzo kimoja ("Answering-Christianity.com) kinachosema " Jihad doesn't always mean a war or battle. Any mean for spreading Islam and the Truth, or to fight for what is right and condemn what is wrong (such as fighting the bad and helping the oppressed even if they were not Muslims) are considered Jihad" - sentensi ya ufunguzi hailingani na madai yake kuwa "Katika Qurani neno "jihadi" halina maana ya mapigano ya kijeshi ". Menginevyo ameleta marejeo yote katika matini yanayothibitisha kinyume ya wazo lake. Tokeo ni makala isiyoeleweka. Kwa sababu hiyo nitarudisha mabadiliko yake, ilhali ninampa kwanza nafasi ya kujibu hapa. Kipala (majadiliano) 18:23, 6 Januari 2021 (UTC)Reply

Maana ya kijeshi ya Jihadi hariri

Kwanini kulazimisha kuwa neno Jihadi maana yake ni Mapigano ya kijeshi, neno Jihadi kwa Kiswahili maana yake ni Jitihada au kujitahidi katika njia ya MwenyeziMungu, hakuna ulazima wa kuwa neno jihadi ni vita. Neno vita kwa Kiarabu si Jihadi bali ni Qatar (قاتل), kwa maana nyingine ni kuua kwenye mapigano. (yaliyotangulia yalitungwa na mtumiaji:JJOSY2000 tarehe 18.01.2021, saa 16:18 )

USHAURI hariri

Kwanini makala za Kiislamu (Waislamu) zisiandikwe na Waislamu wenyewe, kwanini mtu ambaye sio Muislamu ndio aandike nakala za Waislamu, je itafaa kwa Muislamu kuandika nakala za Wakristo. Hii ndio imepelekea ndugu Kipara kuwa na uono hasi kuhusu Uislamu na ndio utaona kwenye ukurasa wa Jihadi ameweka kiungo kutoka (www.jihadwatch.com) tovuti ambayo inapinga na kusema vibaya Uislamu. Je Na Waislamu tukweka viungo kuhusu kuusema vibaya Ukristo je itakuwa sawa? Nini lengo la Kipara kuhariri ukurasa wa Jihadi kama si kupotosha maana na kuweka dhana kuwa Uislamu ni vita na mauwaji, ilihali neno Jihadi halina maana hiyo. (yaliyotangulia yalitungwa na mtumiaji:JJOSY2000 tarehe 18.01.2021, saa 16:18 )

Maana mbalimbali ya neno Jihad hariri

  1. Inaonekana JJOSY2000 hapendi kuona kwamba maana mojawapo ya neno "Jihad" katika Qurani ni kijeshi au kivita. Hapo alibadilisha matini bila kuleta ushahidi wowote kwa madai yake kwamba Jihad haina maana ya kijesi; kinyume chake marejeo ya pekee aliyoleta inathibitisha kwamba Jihad inaweza kutaja pia matendo ya vita (angalia Answering Christianity - Jihad inayosema "Jihad doesn't always mean a war or battle." Menginevyo alibadilisha matini ya makala kiasi kwamba hali ya sasa inasikitisha, maana aliacha marejeo yaliyokuwepo lakini kugeuza maana ya matini kuwa kinyume. Kwa hiyo, kama mtu anafuatilia marejeo atachanganyikiwa maana sasa kuna madai ya kinyume kandokando bila maelezo. Kwa sababu hiyo nitafuta tena mabadiliko yake. Amerudia hatua hiyo mara ya pili, hivyo napaswa kumwonya maana anaingiza uharabu. Nahisi yeye ni mchangiaji mpya hivyo haelewi bado utaratibu hapa ila tunapaswa kukinga wikipedia hii. ---- Kuhusu "ushauri" wake: hii inaonyesha bado hakuelewa wikipedia ni nini. . Hali halisi kuna njia mbalimbali ya kusoma dhana ya Jihadi, na moja ni kijeshi. Kwa msimamo huu kuna marejeo kadhaa katika makala; anayeona marejeo hayo hayana mshiko, aionyeshe hapa kwenye majadiliano kwanza.
  2. Namshukuru JJOSY2000 kwa kudokeza tovuti moja iliyoonyeshwa kama marejeo: "Jihadwatch" kweli haina thamani, ni zaidi mahubiri ya kisiasa. Kwa jumla nimeona haisaidii kukusanya hapa tovuti zinazolenga kushtaki au kutetea mawazo mbalimbali kuhusu jihadi kwa makusudi ya kisiasa au kiitikadi. Nimeondoa yote, badala yake napeleka hapa marejeo ya kujisomea kutoka enwiki kw aimani kwamba chaguo hilo limeshapitiliwa na watu wengi wenye msimamo tofauti kati yao. Kipala (majadiliano) 04:32, 19 Januari 2021 (UTC)Reply
Return to "Jihadi" page.