Majadiliano:Machame
Kusalitiwa kwa Mangi Ngamini na Nduguye Shangali
haririHabari hizi ni sawa na vita katika familia moja.
“Bila mikusanyiko mingi ya hakika ya mambo ya zamani tuyaonayo katika historia, na bila kufahamu vyema hali ya nchi yetu ilivyokuwa hapo kale, basi hatutakua na nguvu za kuendelea mbele nasi tutapata hasara tu. Maana tutakosa kuwa na usawa na ufungamano”.
Pro. S.J.Ntiro katika kitabu cha DESTURI YA WACHAGGA.
Maelezo mengini simulizi za wazee na katika kitabu cha Charles Dundas - Wasahuye-O-Kichagga (Elder of Kilimanjaro) ASILI NA HABARI ZA WACHAGGA na Kathlen M. Stahl katika History of the Chagga people of Kilimanjaro.
Katika utangulizi Chales Dundas anasema “Pia mtasoma humuhumu habari za mambo maovu na ya upuuzi yaliyofanywa na watu wabaya, maana mambo kama hayo yamo katika habari za kila nchi”.
Mangi Sina alikua mateka wa vita akiwa kijana mdogo na majemedari wa vita waliamua wasimthuru na wakampeleka kwa Mangi Ndeserua ili kama akitaka amuue mwenyewe, kitu ambacho Ndeserua hakufanya. Badala yake alimlea katika boma yake na alipoendelea kukua alifundishwa mbinu za vita na baadae alishiriki katika vita kati ya Ndeserua na majirani na kupata mafunzo zaidi huko hadi akawa mpiganaji mzuri na mmoja wa Majemedari.
Jina la Sina linatokana na neno la Kimachame “Hisina ifua” yaani kula nyama kwenye mfupa ambao alikuwa anapewa katika boma la Ndeserua akiwa mdogo.
Hata Mangi Ndeserua alipokuwa mgonjwa aliagiza Majemedari wake wampeleke Sina kuwa Mkuu wa Kibosho na kumwachia baadhi ya Majemedari kwa ajili ya kumlinda, hii ilisababisha manung’uniko makubwa kwani isingewezekana Sina kutawala Walambogo kwani hakuwa boma la Kirenga wala kizazi cha Tatua. Msela – Kiwoso aliamua kumuunga mkono Sina na akajenga boma lake kwa Kiwoso hapa ndipo jina la Kibosho lilipoanza.
Ndeserua akifuatiwa na Sina ndio Mangi waliouwa watu wake zaidi katika Kilimanjaro. Mangi Sina ambaye pia alichukua jina la Ukoo la
mlezi wake Ndeserua Mushi.Katika utawala wake kuua ilikuwa jambo la kawaida kwa mtu yoyote aliyehisi au kuambiwa anavizia kiti chake. Sina hakumbakiza hata mwanae kwani palitokea sherehe na ngoma ilivuma kwa mwanawe kuliko kwake akaamua kumuua. DUNDAS UK 132
Dundas anaeleza ukurasa 124 Sina alianza kuwa na nguvu katika utawala wake na hata kwa majirani akaanza kufanya shauri la kuingia na kuiteka Machame, kwa wakati huo alikuwa hana nguvu za kutosha kupiga Machame.
Charles Dundas anaeleza Ndeserua alikuwa na wake hamsini (50) lakini wana wa kiume watatu (3) ndio waliojulikana.Wakati Ndeserua anaugua wazee wa pande zote walikusanyika mbele ya Ndeserua wakamuomba awachagulie mrithi kwa sababu yeye mwenyewe ana nguvu ya kutawala nchi, naye Ndeserua aliwapa Ngamini kuwa kiongozi wao.
Simulizi za wazee wanasema habari nyingine za kukanganisha ambazo zinaonyesha wazi msimulizi wake alikuwa ni Nasua, ambaye alikuwa Njama wa Ndeserua na alikuwa na ushawishi mkubwa na alitoa maamuzi kwa niaba ya Mangi Ndeserua kwani alikuwa mgonjwa sana kwamba Ndeserua alisema Shangali, ambaye alikuwa na miaka mitatu (3) atasubiriwa ndio awe kiongozi.
Pia Charles Dundas ukurasa 123-124 anasimulia jinsi Ndeserua alivyowaacha Usia wa kwamba atakapokufa kifo chake kitangazwe, na hili ni kinyume na desturi ya Wamangi, Dundas anasema Ndeserua alitamani sana nchi yake iangamie palepale atakapokufa ili watu waseme nguvu za nchi ziliisha alipokufa yeye.
Katika kitabu cha Kathleen M. Stahl History of the Chagga people of Kilimanjaro anasema Nasua ni mtoto wa Kishongu Rengua na ni ndugu ya Mankinga kwa mama mwingine. Na Kishongu alikuwa na uwadui na Mankinga na aliuwawa katika vurugu na watu wa Mankinga.
Katheleen Stahl ukurasa 128 anasema Kekwe Mke wa pili wa Ndeserua alikuwa na Nguvu na anayekubalika na watu wake. Nasua alijifanya anamuunga mkono na yuko pamoja naye kwa kumlagai mke wa pili wa Ndeserua Kekwe na kuziba nguo za vita zenye kuaminika zina nguvu ya kiuchawi. Na kuziamishia kwa Nuya mke wa tano na Ndeserua jambo lililofanya Ndeserua azikwe kwa Nuya mke mdogo badala ya kwa mke
mkubwa. Na siri kubwa ya kifo cha Ndeserua walikuwa nayo Nasua na Nuya.
Baada ya Ndeserua kufariki Sina alianza kuonea kijicho Machame na kuanza kupanga mipango wakati huo Ngamini alikua anatawala mtoto mkumbwa wa Ndeserua, wakati huo Kibosho ilikuwa chini ya utawala wa Machame kwa muda mrefu ndio maana walimweka Sina madarakani.
Kwa muda wa mwaka mzima Sina alijisingizia ugonjwa, hata watu wake wakadanganyika, mwisho ikaaminika Sina amefariki ukurasa 132 Baada ya kuchukua korodani ya ngo’mbe iliyooza na kujifungia ili watu waamini alikuwa anaumwa.
Baadaye Mtu mmoja wa Kibosho alitumwa apeleke habari za kifo cha Sina kwa Muro askari mkubwa wa Ndeserua na baadae Ngamini,Ngamini hakuisadiki habari hiyo lakini Muro akawakusanya askari zake upesi ingawa Ngamini alijaribu kuwazuia, lakini walikwenda Kibosho.
Maelezo ya Kathleen Stahl anasema Ngamini alilala njia ya kwenda Kibosho na kuonya, “akasema hakuna atakaye ondoka bila kumruka kama unataka kwenda”na hukuna atakaye rudi kati yenu, Njama na majemedari wake walipita njia za kujificha na kwenda Kibosho kwakua walikuwa wamelagaiwa, mpaka leo haijulikana Mangi Ngamini alijiuaje mtego huo?Nasua ndio aliokuwa akiamasisha watu kwenda katika msiba huu, ingawa yeye mwenyewe hakwenda.Kitendo hichi kiliingiza Machame katika kadhia na maafa makubwa, yawezekana kabisa walioamini walijua Sina ni kama mtoto wa nyumbani, kwani alilelewa na kukulia Machame kwa Mangi Ndeserua, kwa hiyo Wamachame walikwenda katika msiba nyumbani kwa Mangi Sina Udileya Kibosho.
Majemedari waliofika Kibosho walishambuliwa pasipo kuonywa na ikumbukwe walikuja kwa ajili ya msiba, wengi wao waliangamia na wachache waliobaki kama ilivyo katika maelezo ya Charles Dundas walikimbizwa hadi nyumbani kwa Ngamini na walipofika aliwatia moyo walianza kupigana na Askari na Sina, Wakibosho baada ya kupata baadhi ya mateka walirudi kwao, inadhaniwa jambo hili lilitokea 22 Julai, 1884 ukurasa 133 .
Kathleen Stahl alisema walijaribu kukimbia walishambuliwa katika ndiwa Isie baadaye paliitwa “Malala” maana yake Vita ya Damu. Shambulio hili lilitwa mauaji ya Masengen (Kimachame) au Masenjala,(Kikibosho) mateka walichuliwa baadaye kwa Waarabu
Ndipo watu wakaamini alichokua anasema Mkuu wao Ngamini,msiba mkubwa uliipata Machame watu walifadhaika sana kwani karibu kila familia ilipatwa na msiba.
Baada ya maafa hayo,Ngamini akawaapiza watu wake “wasijenge nyumba na mlango ukaelekea Kibosho na wala wasioe Kibosho wala kuolewa”. Baada ya tukio hili Machame ilikuwa imepoteza Majemedari wengi wa vitu na nguvu ya kivita ikawa ndogo, ikumbukwe kwamba Mangi Sina alilelewa Machame na alikuwa anajua ubora wa Ngamini na Majemedari hao, ambao kwa wakati mwingine alishiriki nao vita, kwa hiyo mpango wa kudhoofisha Machame ili aweze kutawala kwa amani bila kuogopa nguvu ya Machame na kuchukua mateka na mifugo ulifanikiwa kwani pia aliweza kuwagawa baadhi ya jamaa wa Ngamini kuwa upande wake.
Dundas ukurasa 134 anaelezea baada ya hapo Ngamini alijengea Boma Imara (Turuwe) na akalizungusha handaki lililokwenda chini sana, Mangi Sina alipopata habari akatumia jeshi kulibomoa, ukumbuke hapa Majemedari wengi na Machame walishauliwa kwa Sina. Ngamini hakuwa na jeshi kubwa katika kisa hichi,Nasua ambae alikuwepo katika vita hii, kama mmoja wa Askari wakubwa alitoka nje kujisalimisha ili kupata Amani, akatwaliwa kuwa mateka. Wamachame wakaamua kuwatuliza adui kwa kuwapelekea ng’ombe zao zote na Wakibosho wakawatwa Ng’ombe hao pamoja nahayo Wakibosho wakaendelea na vita. Wamachame wakajua Sina anataka kuwaangamiza wao na nchi yao pia, ndipo walipoamua kupigana kwa ghadabu na kufanikiwa kuwafukuza Wakibosho kwa hasira kubwa, Wamachame wakakimbilia msituni na wengi wao waliuwawa.
Sasa Ngamini akaamia katika Boma alilolijenga Muro kabla ya kufa kwake. Wakibosho walimvamia na walishindwa, huko nyuma Nasua aliyekuwa angali mfungwa wa Sina alimsihi Mangi Sina kila siku, asiwaangamize Wamachame na nchi yao kwani akishafanya hivyo hatapata mateka yoyote.
Ukurasa 135 Mangi Sina aliona huruma akamruhusu Nasua aende akamlete Ngamini, lakini Ngamini alimtendea Nasua kama ni adui tu.
Nasua alirudi kwa Sina,Sina akaanza vita tena. Kisha Nasua akamsihi Sina amwite Shangali na kumweka awe Mkuu mahali pa Ngamini. Sina alikubali na kufanya hivyo akampeleka Shangali na jeshi hodari mpaka Machame, akamweka awe Mkuu Machame, Ngamini alizidi kujishikiza katika Boma la Muro mpaka baada ya miezi mitano (5), kwa ushauri wa Missionari Alexander Leroy na Afisa wa Kijerumani aliyekuwa Boma la Moshi aliyeitwa Kapten Eltz,hatimae alikimbilia Moshi kwa Mangi Rindi akapokelewa vizuri.
Palitokea malalamiko Wamachame iliyochochewa na Ngamini na Mnyamari waliojaribu kumshawishi Mangi Rindi awapatie shauri Jema kwa Wadachi kabla Wissmann hajaondoka Kilimanjaro, Wadachi waliyaacha mambo mikononi mwa Rindi akakata Shauri ya kuwa Shangali asiwe mkuu, maana wazee wake walisema Shangali ni chombo tu cha Sina.
Rindi aliona ya kuwa hawezi kumshinda Sina. Ngamini daima alimsihi Rindi kupigana na Shangali ni kupigana na Sina ukurasa 136 Rindi alipeleka wajumbe Pwani akaomba msaada kwa Wadachi. Hapo, basi Bwana askari mmoja wa Kidachi alipelekwa Kilimanjaro kutafuta habari. Rindi akampa habari zote za nchi, lakini hasa alimwambia habari za ubaya wa Sina katika nchi ya Machame, maana siku hizo alikuwa akiwaonea sana kwa sababu alikuwa akishughulika kumshinda Ngamini. Mwishowe Yule Mdachi alikwenda Machame akampa Ngamini bendera ya Kidachi iwe alama ya kuwa nchi yake iko chini ya himaya ya wadachi. Kisha, akamwonya Sina kwamba akiwadhuru Wamachame tena basi ajue kwamba vitatokea vita na Wadachi, aliahidi kuiheshimu bendera ya Wadachi ikawa Yule Mzungu akarejea Pwani. Lakini mara alipokwisha kwenda zake, Sina akaenda Machame akaipasualia mbali bendera ile ya Kidachi, akaichomachoma kwa mikuki.
Ukurasa 142 Major Wissmann alikuja Moshi mwezi 1 Febr, 1890 na siku ya kumi na mbili (12) ya mwezi ule ule akafanya safari kwenda Kibosho. Baada ya vita ya siku mbili Boma ya Sina ilishambuliwa Sina aliokoka baada ya siku mbili alijitokeza na kusamehewa, kwa sharti moja asifanye tena udhia.
Mara baada ya Wadachi kuondoka tena, Sina aliingilia Machame akamweka Shangali awe mkuu tena, Ngamini alikimbilia Moshi. Kathleen M. Stahl ukurasa 124 Mangi Ngamini alibaki kama mkimbizi
Moshi na baada ya muda mchache kupita Ngamini alikufa kwa kuwekewa sumu katika Tumbaku kama zawadi kutoka Machame kwa maelezo ya Kathleen M. Stahl katika kitabu chake na ilikuwa kati ya mwaka 1890. Ukurasa 101. Katika chati ya utawala wa Machame Ngamini alitawala mwaka 1870 mpaka 1889 ndiye Mangi pekee aliyekuwa na huruma tofauti na Baba yake Mangi Ndeserua
Page 101 Kathlen M.Stahl history of Chagga people Kilimanjaro
Shangali alibaki Mkuu wa Machame akisaidiwa sana na washauri wake Nasua na Karawa, Wakibosho wakati huo hawakutaka Wamachame wafanikiwe, walimuomba Sina asiruhusu wakawa matajiri na wenye nguvu wataasi, Sina akawaita Nasua na Karawa na kuwafunga, akawashambulia Wamachame kwa ghafta akawaua watu wengi, wala hakuwa na hurumia hata wanawake na watoto.
Charles Dundas ukurasa 143-144 Sina akamwita Shangali, Shangali hakufanya makuu ila alikwenda kwa Sina akamwona hataki kuasi
akaahidi awe rafiki yake na mlinzi,basi walichinjiana udugu na Shangali alipewa ruhusa arudi kwake. Sina akampa Ng’ombe wakae kwake yaani ni dalili ya kuwa nchi ya Shangali ni chini ya ulinzi wake, wazee wanasema kitendo hicho alichofanya na Mangi Sina kuweka Udugu na Mangi Shangali mdogo wake Ngamini ni kufuta yote ambayo Machame ilitendewa na Mangi Sina na kufuta yale ambayo Kibosho ilitendewa na Mangi Rengua. Kuanzia hapo Machame ikawa katika Amani.
February 1881 Utawala wa Kidachi wakishirikiana na Jeshi la Mangi Rindi walishambulia Boma ya Sina ukawa ndio mwisho wa nguvu ya Sina, na alifariki mwaka 1897 na alitawala toka mwaka 1970 mpaka 1877.Baada ya ujio wa Wadachi Mangi hawakuwa na nguvu waliitwa Chief na hawakuwa na uwezo wa kuamua mambo yao wenyewe bila kuridhiwa na Wazungu.
Page 157 Kathlen M.Stahl history of Chagga people Kilimanjaro
Serikali ya Kidachi baada ya uchunguzi wa kifo cha Mangi Ngamini walirudisha familia yake katka makazi yao ya asili Machame na fuvu la kichwa cha Mangi Ngamini.
Katika kitabu cha DESTURI YA WACHAGGA kilichoandikwa naPro. S.J.Ntiro kinaeleza vita kati ya Wamangi ilikuwa vibaya kwa kuwa badala ya kuunga nguvu zao ili nchi iendelee mbele, iliwabidi kutumia nguvu nyingi wakipigana wenyewe kwa wenyewe. Watu walichimba mahandaki marefu ambayo yaliwachukua muda mrefu.
Pamoja na lawama nyingi alizopewa Sina baada ya tukio la kujisingizia amekufa na kuangamiza Wamachame, ikumbukwe babu yake Mangi Rengua yaani baba yake Mankinga. Mangi Rengua aliwahi kufanya hila kama hiyo wakati Kibosho inanjaa, aliwadanganya Wakibosho akasema mambo yote yatatokea vizuri ikiwa vijana wa Kibosho watakuja Machame kucheza unyago wa Ngashi. Mangi Kashenge akakubali, akawapeleka vijana wake katika mto Marire palipokuwa pameandaliwa. Walipoanza unyago watu wa Rengua wakawashambulia vijana wasiokuwa na silaha kwa ghafla wakawauwa hakuna hata mmoja aliyesalia, tendo hili lilianzisha chuki katika nchi hizi mbili. Maelezo haya yapo katika kitabu cha Charles Dundas ukurasa 84.
Maswali ya kujiuliza juu ya historia hii
- Je Mangi Sina alikuwa akilipa kisasi kwa ajili ya yaliyofanywa na Mangi Rengua?
- Je Mangi Sina aliamua kuvunja nguvu ya Machame kwa kushirikiana na ndugu za Mangi Ngamini ili asiwe chini ya utawala wa Machame waliomweka madarakani?
- Je huu ulikuwa mpango wa Nasua ambae akutaka Mangi Ngamini atawale?
- Je huu ulikuwa mpango wa Mangi Ndeserua nchi yake iangamie palepale afapo? Charles Dundas uk.124
“Siku hizi tunaweza kusafiri toka pembe hata pembe ya nchi hii pasipo hofu ya watenda maovu, basi imetupasa kufikiri vyema kuwa kila mahali tunapokanyaga sasa, zamani palikuwa mahali pakuharibia na kuuana na kutesana” mahali kwenye chuo cha Machame cha sasa ndipo Ndeserua alipokuwa akiwachinja raia zake pasipo huruma na kufanya shauri la kuiangamiza nchi yake mwenyewe kabla hajafa. Tungalikuwa
tukiishi siku zile, pia tungaliweza kumwona Mangi Sina, mwenye ghadhabu akiwachinja watu na kuleta uharibifu katika nchi kutoka mahali kilipo chuo cha Moshi alisema Charles Dundas.
“Yaliyopita si ndelwe, Tugange yajayo”.
“INGAWA TAYARI MILANGO YA NYUMBA INAELEKEA KIBOSHO NA MACHAME NA WATU WANAOANA”
Mwandishi wa nakala hii ni mtoto wa Baba wa Kimachame na Mama wa Kikibosho baada ya kukosa ukweli huu kwa kuongea na wazazi aliamua kutafuta ukweli huu wa kusoma vitabu na kuongea 197.250.130.250 08:27, 16 Februari 2024 (UTC)