Majadiliano:Moyo

Latest comment: miaka 8 iliyopita by Lucas559 in topic Marejeleo

Zaidi bidhaa kutoka EN Wikipedia, iliyotafsiriwa na Watafsiri wasio na mipaka.

Kigezo:Infobox anatomy Moyo ni kiuongo chenye chenye misuli katika binadamu na wanyama wengine, ambacho hupiga damu kupitia mishipa ya damu ya mfumo wa mzunguko wa damu.[1] Damu huupatia mwili oksijeni na virutubishi na pia husaidia katika utoaji wa uchafu wa umetaboli.[2] Moyo huwa katika sehemu ya katikati ya mediastinamu katika kifua.[3]

Katika binadamu, mamalia wengine na ndege, moyo umegawanywa katika sehemu: sehemu ya juu ya kushoto na kulia atriamu; na sehemu ya chini ya kushoto na kulia ventrikali.[4][5] Mara nyingi, atriamu na ventrikali za kulia kwa pamoja hujulikana kama moyo wa kulia nao upande wa kushoto kama moyo wa kushoto.[6] Kinyume na hivi, samaki huwa na chemba mbili, atriamu na ventrikali huku reptilia wakiwa na chemba tatu.[5] Katika moyo wenye afya, damu hutiririka kwa njia moja kupitia katika moyo kwa sababu ya vali za moyo, zinazozuia kurejea kwa damu.[3] Moyo huwa umefunikwa katika kifuko cha kuzuia cha perikadiamu ambacho pia kina kiasi kidogo cha kiowevu. Ukuta wa moyo huwa na safu tatu: epikadiamu; miokadiamu; na endokadiamu.[7]

Moyo hupiga damu kwa mifumo yote miwili ya mzunguko wa damu. Damu yenye uhaba wa oksijeni kutoka kwa mzunguko wa kimfumo huingia kwenye atriamu ya kulia kutoka kwa mshipa wa juu na mshipa wa chini vena kava na kupita hadi kwenye ventrikali ya kulia. Kutoka hapa, damu hii hupigwa hadi katika mzunguko wa damu kwenye mapafu,kupitia katika mapafu ambapo hutiwa oksijeni na kutolewa dioksidi ya kaboni. Damu yenye oksijeni kisha hurejea katika atriamu ya kushoto, na kupitia katika ventrikali ya kushoto kusha kupigwa nje kupitia katika aota hadi katika mzunguko wa kimfumo ambapo oksijeni hutumika na kumetaboliwa hadi dioksidi ya kaboni.[2] Kwa kawaida katika kila mpigo wa moyo, ventrikali ya kulia hupiga kiasi sawa cha damu hadi katika mapafu sawia na kiasi kinachopigwa nje hadi kwenye mwili na ventrikali ya kushoto. Vena husafirisha damu hadi kwenye moyo huku ateri zikisafirisha damu hii kutoka kwenye moyo. Mishipa kwa kawaida huwa na shinikizo la chini kuliko la ateri.[2][3] Moyo hukazana kwa kiasi cha takriban midundo 72 kwa kila dakika wakati wa mapumziko.[2] Mazoezi huongeza kiasi hiki kwa muda mfupi, lakini hupunguka kiasi cha mdundo wa moyo katika mapumziko mwishoni na hili hunufaisha moyo.[8]

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (CVD) yalikuwa kisababishi kikuu zaidi cha vifo ulimwenguni kote mwaka wa 2008, hii ikiwa ni asilimia 30 ya visa vyote.[9][10] Kwa vifo hivi vyote, zaidi ya robo tatu vilisababishwa na ugonjwa wa ateri ya koronari na kiharusi.[9] Vipengele vya hatari vinajumuisha: uvutaji sigara, kuwa mnene kupindukia, kutofanya mazoezi ya kutosha, viwango vya juu vya kolestroli, shinikizo la juu la damu, na kisukari usiodhibitiwa vyema.[11] Utambuzi wa ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hufanywa kwa kusikiliza sauti ya moyo kwa kutumia vipimo vya juu sana vya sauti, ECG au kwa ekokadiogramu.[3] Magonjwa ya moyo kimsingi hupimwa kwa wakadiolojia, ingawaje wataalamu wengine wa kimatibabu wanaweza kuhusika.[10]

Marejeleo hariri

  1. Taber, Clarence Wilbur; Venes, Donald (2009). Taber's cyclopedic medical dictionary. F a Davis Co. pp. 1018–23. ISBN 0-8036-1559-0. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Hall, John (2011). Guyton and Hall textbook of medical physiology (12th ed. ed.). Philadelphia, Pa.: Saunders/Elsevier. p. 157. ISBN 978-1-4160-4574-8.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Guyton" defined multiple times with different content
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Keith L. Moore; Arthur F. Dalley; Anne M. R. Agur. "1". Clinically Oriented Anatomy. Wolters Kluwel Health/Lippincott Williams &Wilkins. pp. 127–173. ISBN 978-1-60547-652-0. 
  4. Cecie Starr; Christine Evers; Lisa Starr (2 January 2009). Biology: Today and Tomorrow With Physiology. Cengage Learning. pp. 422–. ISBN 978-0-495-56157-6. Retrieved 7 June 2012. 
  5. 5.0 5.1 Reed, C. Roebuck; Brainerd, Lee Wherry; Lee,, Rodney; Inc, the staff of Kaplan, (2008). CSET : California Subject Examinations for Teachers (3rd ed. ed.). New York, NY: Kaplan Pub. p. 154. ISBN 9781419552816. 
  6. Phibbs, Brendan (2007). The human heart: a basic guide to heart disease (2nd ed.). Philadelphia: Lippincott Williams & Wilkins. p. 1. ISBN 9780781767774. 
  7. Betts, J. Gordon (2013). Anatomy & physiology. pp. 787–846. ISBN 1938168135. Retrieved 11 August 2014. 
  8. Hall, John (2011). "84". Guyton and Hall textbook of medical physiology (12th ed. ed.). Philadelphia, Pa.: Saunders/Elsevier. pp. 1039–1041. ISBN 978-1-4160-4574-8. 
  9. 9.0 9.1 Cardiovascular diseases (CVDs) Fact sheet N°317 March 2013. World Health Organization. Iliwekwa mnamo 20 September 2014.
  10. 10.0 10.1 Longo, Dan; Fauci, Anthony; Kasper, Dennis; Hauser, Stephen; Jameson, J.; Loscalzo, Joseph (August 11, 2011). Harrison's Principles of Internal Medicine (18 ed.). McGraw-Hill Professional. p. 1811. ISBN 9780071748896. 
  11. Graham, I; Atar, D; Borch-Johnsen, K; Boysen, G; Burell, G; Cifkova, R; Dallongeville, J; De Backer, G; Ebrahim, S; Gjelsvik, B; Herrmann-Lingen, C; Hoes, A; Humphries, S; Knapton, M; Perk, J; Priori, SG; Pyorala, K; Reiner, Z; Ruilope, L; Sans-Menendez, S; Scholte op Reimer, W; Weissberg, P; Wood, D; Yarnell, J; Zamorano, JL; Walma, E; Fitzgerald, T; Cooney, MT; Dudina, A; European Society of Cardiology (ESC) Committee for Practice Guidelines, (CPG) (Oct 2007). "European guidelines on cardiovascular disease prevention in clinical practice: executive summary: Fourth Joint Task Force of the European Society of Cardiology and Other Societies on Cardiovascular Disease Prevention in Clinical Practice (Constituted by representatives of nine societies and by invited experts).". European heart journal 28 (19): 2375–414. PMID 17726041. doi:10.1093/eurheartj/ehm316. 

Lucas559 (majadiliano) 18:37, 17 Agosti 2015 (UTC)Reply

Return to "Moyo" page.