Majadiliano:Pasifiki

Pasifiki ni bahari kubwa kuliko zote duniani.

Pasifiki iko kati ya Bara la Amerika upande wa mashariki na Bara la Asia / Australia upande wa magharibi.

Eneo lake ni kilometa za mraba milioni 179.7 ambayo si bahari kubwa tu bali pia ni eneo kubwa kuliko nchi kavu yote duniani: ni karibu nusu ya uso wa dunia.

Kuna visiwa zaidi ya 25,000 katika bahari ya Pasifiki; vingi ni vidogo sana. Visiwa hivyo huhesabiwa mara nyingi pamoja na Australia kama "Australia na Pasifiki".

Pasifiki ina kina cha wastani wa mita 4,028; kina kirefu katika mfereji wa Mariana kinafikia mita 11,034. Pasifiki inavyoonekana kutoka angani; Australia iko upande wa kushoto chini.

Bahari za pembeni ziko hasa upande wa Asia / Australia. Kati ya hizo ni: Bahari ya Celebes, Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China.

Jina la Pasifiki (kwa Kilatini: ina amani, yaani kimya) limetokana na Wazungu wa kwanza waliovuka bahari hii mwaka 1520 BK kutoka Amerika ya Kusini hadi Ufilipino wakaikuta kuwa ni bahari tulivu sana kuliko bahari yoyote.

Lakini Pasifiki inaweza kuwa na dhoruba kali sana. Ni eneo lenye matetemeko ya ardhi mengi yanayosababisha mawimbi haribifu ya tsunami ambayo yanamaliza miji na vijiji vyote vilivyo ufukoni.

Return to "Pasifiki" page.