Majadiliano:Shairi


Katika ushairi, tutaangalia:


KIPENGELE

MAELEZO KWA UFUPI


Aina za Mashairi

Kuainisha mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.


Bahari za Ushairi

Muundo wa shairi kulingana vina, idadi ya mizani, vipande, mpangilio wa maneno n.k.


Uchambuzi wa Mashairi

Mambo muhimu unayohitajika kuzingatia unapochambua shairi


Uhuru wa Mshairi

Ukiukaji wa kanuni za sarufi


Istilahi za Kishairi

Msamiati unaotumika katika ushairi km vina, mizani n.k


Sifa za Ushairi

Sifa zinazobainisha ushairi kutokana na aina nyingine za sanaa.


Umuhimu wa Ushairi

Umuhimu wa ushairi katika jamii.




Istilahi za Kishairi

Haya ni baadhi ya maneno ambayo hautakosa kukutana nayo unapozingatia ushairi. Ni muhimu mwanafunzi kuyajua vizuri. 1.Shairi - ni sanaa ya maneno (utunzi maalum wa lugha ya kisanaa) unaotumia mpangilio na uteuzi maalum wa maneno na sauti ili kupitisha ujumbe fulani.

2.Vina - ni silabi za mwisho katika kila kipande.
3.Mizani - ni idadi ya silabi katika kila mshororo.
4.Mshororo - ni msitari mmoja wa maneno katika shairi.
5.Ubeti - ni kifungu cha mishororo kadhaa.
6.Vipande - ni visehemu vya mshororo vilivyogawanywa kwa alama ya kituo(,)
7.Ukwapi - kipande cha kwanza katika mshororo
8.Mwandamo - Kipande cha tatu katika mshororo
9.Ukingo - kipande cha nne katika mshororo
10.Utao - kipande cha pili katika mshororo
11.Mwanzo - mshororo wa kwanza katika ubeti
12.Mloto - mshororo wa pili katika ubeti
13.Kimalizio/Kiishio - mshororo wa mwisho katika ubeti usiorudiwarudiwa katika kila ubeti.
14.Kibwagizo - mshororo wa mwisho katika ubeti unaorudiwarudiwa kila ubeti.



Sifa za Ushairi 1.Huwa na vina, mizani, mishororo na beti 2.Hutumia lugha teule 3.Hufupisha au kurefusha maneno ili kutosheleza idadi ya mizani 4.Mashairi hayazingatii kanuni za kisarufi. (Angalia uhuru wa mshairi) 5.Hutumia mbinu za lugha



Umuhimu wa Mashairi 1.Kuburudisha 2.Kuhamasisha jamii 3.Kukuza sanaa na ukwasi wa lugha 4.Kuliwaza 5.Kuelimisha 6.Kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza 7.Kupitisha ujumbe fulani 8.Kusifia mtu au kitu 9.Kukejeli au kukemea mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii

Start a discussion about Shairi

Start a discussion
Rudi kwenye ukurasa wa " Shairi ".