Majadiliano:Tanzu za fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina tanzu kuu nne(4)
- hadithi
- semi
- ushairi
- sanaa za maigizo\sanaa za maonesho
hadithi hariri
ni tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupifupi zitumiazo lugha ya nadharia.
semi hariri
ni fungu za tungo za fasihi simuliziambazo ni fupifupi zenye kutumia picha tamathali na semi ya ishara.
ushairi hariri
ni fungu la fasihi simulizi linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo yenye utaratibu maalumu.
sanaa za maigizo\sanaa za maonesho hariri
Ni sanaa zinazoambatana na utendaji wa vitendo vya wahusika mbele ya hadhira.mfano michezo ya majukwaani.
sifa za tanzu za fasihi simulizi hariri
- kufa
- kuzaliwa
- kukua.
kila tanzu ina vipera vyake
vipera vya hadithi hariri
- Ngano
- Vigani
- Visasili
- Tarihi
- Soga
vipera vya semi hariri
- Methali
- Vitendawili
- Nahau
- Misemo
- Mafumbo
- Lakabu
- Mizungu
vipera vya ushairi hariri
- Shairi
- Utenzi
- Nyimbo
- Ngonjera
- Maghani
vipera vya maigizo hariri
- Majigambo
- Vichekesho
- Kuigiza
- Mivigha\miviga
- Ngoma