Majadiliano:Tawimto

Latest comment: miaka 4 iliyopita by Kipala in topic Tawimto: ngeli na uwingi

Tawimto: ngeli na uwingi hariri

tulikuwa na majadiliano kama "tawimto" (istilahi hii ni pendekezo kutoka "Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia" ya 1995) iwe upande wa "tawi" (yaani tawimto la, uwingi matawimto) au upande wa "mto" (yaani tawimto wa, uwingi tawimito) Jibu kutoka Dr Hans wa Tataki ni: "Kuhusu suala la umoja na wingi. hapo inategemea msisitizo uko wapi. Katika mukhtada huo, nafikiri matawimito ni muafaka zaidi". Kipala (majadiliano) 18:51, 1 Novemba 2019 (UTC)Reply

Asante kwa juhudi zako, ila matawimito ni kama jumla ya matawi mengi ya mito mingi. Mwanakijiji wingi wake ni wanakijiji. Ukisema wanavijiji watu watakushangaa, pia baada ya kufikiri wataelewa unamaanisha watu wa vijiji mbalimbali.

Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:21, 8 Novemba 2019 (UTC)Reply

Nimepata nafasi tena kuuliza watu wengine pale Tataki (pamoja na huy aliyeshiriki katika warsha). Baada ya kujadiliana kidogo walisimama upande wako. Basi, matawimto! (Niliuliza kuhusu UKIMVI, wamkubali nami atika mantiki "virusi ya" lakini walisema uzoefu umeshaendelea, basi "Kirusi - Virusi". Halafu "Vita" ni "ya", si "vya". Kipala (majadiliano) 06:52, 9 Novemba 2019 (UTC)Reply
Return to "Tawimto" page.