Majadiliano:Tuzo ya Nobel
Latest comment: miaka 12 iliyopita by Abbasjnr in topic Nobeli au Nobel
Nobeli au Nobel
haririSalaam, nadhani neno "Nobel" linapaswa kuwachwa vivyo hivyo, sio "Nobeli" kwa maana ni jina la mtu. Abbasjnr (majadiliano) 08:38, 11 Septemba 2012 (UTC)
- Ndugu Abbas, nakubali asilimia mia moja nawe. Nilipoanzisha makala hizo miaka ya 2006 na 2007 nilitumia "Tuzo ya Nobel". Baadaye nilipigiwa vita ya uhariri na mtu fulani (nimesahau jina lake), naye akabadilisha makala zote kuwa "Nobeli". Halafu wahariri wengine wakaniunga mkono nasi tukarudisha mabadilisho hayo - angalia makala na jamii za Tuzo ya Nobel kwa mada fulani, k.m. http://sw.wikipedia.org/wiki/Tuzo_ya_Nobel_ya_Fasihi - ila inaonekana tumesahau makala hiyo kuu. Asante kwa kunikumbusha. Naibadilisha sasa hivi. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 09:44, 11 Septemba 2012 (UTC)
- Ahsante. :-) Pia, ngeli ya "tuzo" ni gani? Je, inafaa kuwa "tuzo la Nobel" au "tuzo ya Nobel"? Abbasjnr (majadiliano) 06:03, 12 Septemba 2012 (UTC)
- Katika kamusi ya TUKI ilivyoandikwa ni ifuatavyo: tuzo nm [i-/zi-] prize, reward. Maana yake, tuache "Tuzo ya Nobel" na tusiibadilishe kuwa "Tuzo la Nobel" hata kama wengine wangeandika tuzo nm [li-/ya-] prize, reward. Sawa? --Baba Tabita (majadiliano) 07:11, 12 Septemba 2012 (UTC)
- Tena, ukitafuta "tuzo hii" katika Google utapata matokeo 5,490 kulingana na matokeo 145 tu kwa "tuzo hili". Vilevile, matokeo 2,460 kwa "tuzo hizi" na matokeo mawili tu kwa "matuzo haya". Haya! :) --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 12 Septemba 2012 (UTC)
- Ahsante. :-) Pia, ngeli ya "tuzo" ni gani? Je, inafaa kuwa "tuzo la Nobel" au "tuzo ya Nobel"? Abbasjnr (majadiliano) 06:03, 12 Septemba 2012 (UTC)