Majadiliano:Ukristo

Latest comment: miaka 16 iliyopita by Moses in topic Makala hii ya sasa
Naomba kurasa za majadiliano zisisogezwe. Asante! --Oliver Stegen 15:32, 30 May 2007 (UTC)

Majibu ya Moses kwa Eddy Albert tarehe 20-23 Mei, 2007

hariri

Ukristo ni mfumo wa mapokeo kuhusu Mungu, Kristo na Mamlaka. Hii imeleta utamaduni wa Kanisa na waumini. Chimbuko la Ukristo ni kuwepo kwa mtu aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko Mashariki ya Kati, katika nchi ya Nazareti iliyopo hadi hii leo kwenye mipaka ya Israeli. naye alikuwa akiitwa Yesu Mnazareti, mwana wa Yosefu mchonga samani. mama yake akifahamika kwa Jina la Mariamu.

Asili ya Ukristo hasa ni matokeo ya uzaliwa wa Yesu, uliopekelewa miongoni mwa walioona kwamba yeye mi Masiya; yaani mkombozi. yeye alikuwa timilizo la ahadi za koo za mstari wa uzao wa manabii ulioanziwa na Musa. Musa alikuwa mwana matengenezo ya kijamii aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka Utumwani misri takribani miaka 4000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu. Musa alikuwa ni wa kwanza kutabiri kuja kwa masiha atakaye wakomboa waisraeli kutoka katika kile kilichofahamika kwa nje kama mwana kondoo ataye safisha mizigo ya dhambi na tena mpatanishi kati ya Mbingu na Nchi yaani Wanadamu na Mungu. Na kwamba kuja kwake ni agano Jipya. Kwani Musa aliikuwa ni wa kuaanzisha Agano lenye kutangulia; yaani la Kale. Hivyo Musa alikuwa kiongozi aliye kabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia watakao shikilia Agano la kusubiri Masiya kushirikiana na Manabii na Makuhani.

Musa alikuwa ni Mmajia, yaani mtu mwenye maarifa, hekima na busara kutoka kwa Makuhani na Mamistiya wa Kimisri. Kwani Musa alilelewa katika nyumba ya kifalme ya Misri baada ya kuopolewa majini na kijakazi aliyeagizwa na malkia kufanya hivyo baada ya malkia kupewa taarifa ya mtoto wa kiisraeli aliyeonekana kutelekezwa. Naye malkia alivutiwa na uzuri wa mtoto na akaagiza atuzwe vizuri lakini abaki kuuishi katika jumba la kifalme. kama ililiyokuwa kztika siku zile; Musa alilelewa kwa mujibu wa desturi zote za koo za kifalme. Wenye Hekima na Maona kutoka kwenye nyanja mbali mbali za elimu na ilimu yaani maarifa ya jamii na maarifa ya ndani kuhusu siri za mbingu na Nchi. Naye Musa akajifunza mambo mengi kuhusu umistiya na majia yaani maarifa ya kubadili maumbo, sura na sifa ya vitu na hata Akili na Nafsi kwa kutumia ilimu ya njia za siri zenye kusababisha mabadiliko ambayo wengine wangeweza kuona kama ni mazingaombwe. Na hiyo ndiyo hekima halisi yaani Majia.

Naye Musa akiwa kama binadamu mwenye moyo wa uzalendo na kupenda asili yake; alikerwa na maisha ya kuona ndugu zake wa kiisraeli waiishi na kunyanyasika ughaibuni. Hivyo akakusudia kufanya hima awakomboe waisraeli kutoka kwenye mikono ya wamisri. Kutokana na matukio kadhaa yaliomsibu; Musa aliamua kwenye kuishi mpweke milimani akitafakari na kuzama kwenye ilimu na majia katika nia ya kutafuta Uweza utakao mwezesha kumpa nguvu ya kuwakomboa waisraeli. Kwa maarifa yake na majaribio yake pamoja utahayari wake; Musa alifanikiwa kukaribisha Uwepo mmoja uliokuja katika sura ya moto. Kuna elementi nne za msingi zinazowakilisha mbingu na nchi yaani mambo ya Juu na Mtu ama Dunia. Jua na Mwezi; Kama ilivyo Juu ndivyo ilivyo Chini. Musa alijua siri kutoka mamistiya wale wa siku alizokuwa akiishi kwenye Jumba la kifalme. Nazo hizo elementi ni Udongo, maji, Hewa na Moto. Moto ikiwa ni nguvu yaa juu zaidi yenye kuweza kubadili vyote vyenye kufanyika kutokana na asili ya Ardhi na Hata Moto. Na hii ndo siri ya Musa kuwashinda wachawi na waganga wa kimisri wa siku zake aliporudi Kwa Mtawala wa kimisri na kutaka Uhuru wa watu wake. Mfalme wa kimisri alimpambanisha na hao, naye akawashinda. Hilo lilikuwa shauri la thibitisha hekima kuu kuzidi ya wamisri kwani miaka hiyo Hekima yenye kusababisha nguvu kuu ilikuwa ikisadikiwa kutoka kwa Mungu mkuu. Na kila jamii ilikuwa na wenye Busara wao walioategemea na kusadiki yote walioambiwa na wao, ya kwamba yanatoka kwa Mungu wao. Hivyo taswira ya Mungu katika zama zile ilikuwa ni ubinafsishaji wa uweza mkuu katika kukinga na kustawisha jamii husika. Na hiyo ndio taswira ya kale ya Binadamu kuhusu yale yaliyo Juu. Kwani Majia wanajua kuna mambo ya chini na ya Juu. Binadamu yupo ukingoni mwa ya chini katika kuchagua Mambo ya Mbingu ama Nchi. Musa aliwaeleza waisraeli habari za Mungu mkubwa mwenye kuwaongoza kuelekea kwenye ufalme mkuu... Lakini kwa kweli ile haikuwa kweli kamili kwani matokeo yanaonekana hadi hii Leo. Musa hakuwa na jinsi. Watu wa kale walifaa kwa mambo ya kikale; ila moyoni mwake alijua ukweli kwamba nchi ya ahadi si mahala pa kufikia kwa namna ya nchi, bali ni kwa roho kwani mamajia wote wa zama zote walilifahamu hilo katika ngazi fulani utambuzi wao. Hivyo Musa, baadae, baada ya kuuona itachukua vizazi na vizazi kwa wana wa israeli kuelewa mambo ya kiroho, alitoa ahadi ya masiha na kukabidhi kwa waliomfuatia yaani viongozi wa waisraeli mara baada ya yeye kuamua kwenda zake milimani ambako ilidhaniwa alifia huko. na Ukweli hakuna kaburi lake hata huko milimani, na hakuna aliyejua Musa alifia wapi hasa kwa siku zile.

Basi kuna mambo mengi yaliyotokea siku zile za wana wa Israeli kuuondoka Utumwani na kuelekea Nchi ya Ahadi. Miaka mingi ilipita na Musa alianza kukata tamaa na baadhi ya maelekezo kutoka kwa Mungu aliyempa uwezo aliianza kutokutii. Ilikuwa ni kana Kwamba kuna Kosa ambalo yeye wenyewe hakudhania wala kutegemea kuhusu ushirikiano wake na Mungu huyo. Hivyo jitahada ya pili ni kuandaa kuzaliwa kwa masiha, yaani mkombozi halisi. Naye atazaliwa na hatimaye kuwa nguvu kamili ya kuleta badiliko kutoka ndani yake. Yaani asiyetumia namna za nje kuleta mabadilika isipokuwa uwezo wa ndani. Yaani kufanyika. Hivyo siri ya masiha ilijulikana vizuri miongoni mwa manabii wengi israeli ambao kweli walijua maarifa mengi kuhusu jinsi kupata maono kupitia Njozi na hata utuliviu wa Akili ikienda sambamba na neema pia kiu yao ya kutumikia jamii kiroho. Hivyo, nabii Isaya ni mmoja aliyetoa tafsiri bora kabisa na ya moja kwa moja kuhusu Masiha katika kitabu chake lilichopo miongoni mwa vitabu vya Biblia; inayochukuliwa kwamba ni kitabu kitakatifu miongoni mwa Wakristo. Isaya 11:1-7 inazungumzia kuhusu Masiya atakayezaliwa kutoka kwenye shina la Yese. Naye Atakuwa mwenye Kuamua kwa busara isiyo kama ile ya watu wa kawaida. Naye ataamua kwa Haki. Tena baada ya Hapo, Nabii Isaya anazungumzia kuhusu Nchi Mpya na Mbingu yenye uzuri na Utukufu... Kitu ambacho kwa kweli hakikutokea. Kwani Siri ya Mbingu Mpya na Nchi Mpya hufuata Ufahamu uliobadilika kitu ambacho huuitwa Kuzaliwa tena Kiroho...

Yesu alizaliwa miaka kama 4000 baada ya Musa. Hiyo ni miaka kama 2000 ilipopita kwani kalenda huhesabu miaka kutoka mwaka wa kuzaliwa kwa Yesu na ndio mchango wa Ukristo uliotapakaa hapa duniani.

Kitabu cha Yohana, yaani Injili ya Yohana huunza na utangulizi wenye fumbo lenye maana kubwa. Ifahamike kwamba mwandishi wa Injili hiyo aliindika miaka mingi baada ya kufariki kwa Yesu hayumkini akizingatia yale aliyoyaona na kujifunza Kutoka kwa Yesu ambaye yeye alimtambua kwamba ni Kristo. Naye anaanza Injili kwa kuzungumzia Neno. Itambulike kwamba Neno ni like kinachotamkwa ama Sauti. Hii ina fanana na mafundisho mengi ya Mashariki yanasema kwamba ulimwengu ni mfanyiko wa Sauti na kwamba kila kitu ni mfano wa sauti yaani nishati fulani ya Nuru itetemayo. Hivyo ulimwengu wote wa sura yaani maada ni nishati inayobeba maksudi ya kuumba. Hivyo nishati hiyo ni yeye utashi na Hai. Utashi na Nia ni sifa Kiumbe hai kinachoweza kuwepo kama kizio yaani umoja. Hivyo asili ya Neno ni mwanzo na ni Mungu kwa maana Asili. Na hii ni siri ya mbingu na pia siri na ya wanadamu. Na huu ndo uzima anaozungumzia Yohana. Kwani mamistiya wanatambua kwamba Ufahamu ni nuru inayo ongoza nafsi katika safari ya kuelekekea Uzima usiokoma, yaani mwanzo na mwisho. Na huo utashi ni mwenge wenye kumfanya mtu atambue kati ya Aliyokwishayajua na yale Atakayoyajua katika kipindi ambacho anaishi na kuchagua na kutenda.

Pia Injili hiyo anamtaja mtu aliitwa Yohana. Yeye anasemwa kwamba alikuja ili aishuidie ile Nuru. Nuru ni kitu gani? Nuru isemwayo hapa ni ufahamu ushindao ule wa mwanadamu wa kawaida unakuja kwa kuzaliwa ndani ya mtu alijiandaa kuupokea. Ifahamike neno Kristo lina maana ya Jiwe. Ama kusema, mwamba wenye kupitisha Nuru kuu bila ya kupinga ama kusharabu. Ni alama ya usafi wa mpitisho wenye kuleta ufasha wa kuona yaani utambuzi. Ifahamike kwamba, hii inafanana na mafundisho ya Ubuddha uliotapakaa huko Tibeti ukitaja kuhusu Akili ya Almasi ya Buddha yenye uwezo wa kupenya na kuelewa siri zote za ulimwengu kutoka mwanzo na hata Mwisho.

Yohana alitabiriwa katika Malachi 4:4 kwambwa atakuja Eliya nabii kabla ya haijaja siku ya Bwana... Na wafuasi wa Yesu walimuuliza Yesu kuhusu huyo Eliya ni Yohana mbatizaji, aliyekamatwa na kufungwa na Herode kwa matakwa ya binti Herodi? Naye Yesu akazia kwamba ndivyo katika Yohana 11:14. Sasa inawezekanaje kwamba yule Eliya nabii kuwa ni Yohana. Hiki ni kati ya vielelezo adimu vilivyomo kwenye Biblia vyenye kuonyesha kwamba Roho ya mtu huweza kutwaa mwili tena na kuzaliwa kupitia tumbo la mwanamke. Inasadikika injili za mwanzo zilikuwa na mifano mingi ambapo Yesu mwenyewe alizungumza hivyo wazi wazi kwa wanafunzi wake. Ndio maana kuna wakati walimuuliza kama mtu kuzaliwa na mapungufu kimaumbile ni matokeo ya dhambi alizotenda kabla kuzaliwa mahala pengine(?). Hivyo Yohana aliishi na kuenenda na roho ya Eliya yule yule alipata kuwepo siku za Nyuma. Hii ni dalili ya kwamba roho hupitia mzunguko wenye kubeba tohara na mafunzo na kutakasika kufikia kioo madhubuti cha Utukufu wa Uliondani, yaani utukufu wa mbingu. Upande wa majia wa maisha ya hapa duniani ni wenye kuweza kuleta majia na hata kubadili hali mbaya za masumbuko na kukata tamaa kuwa utukufu wa juu usio na kasoro. Hivyo siri ya Kristo ni kuleta mbingu mpya na nchi mpya kupitia kiungo cha kristo. Ndio maana Neno; katika utangullizi wa Yohana una sura mbili Yesu kama binadamu na Yesu aliye Kristo yaani aliyezaliwa mara ya pili kwa roho. Na yeye Yohana mwandishi anakili alimwona Yesu kama neno halisi atokaye kwa Mungu na tena aliyejaa neema na Kweli ( Yohana 1:1-14 ).

Ahadi ya Musa kuhusu Kristo ilikuwa ni yenye kutegemea sana Wana wa Israeli watampokeaje Masiha. Ikiwa watambua; basi agano lake lingelitimilizwa na mambo ya kale yangelilikoma. (Paulo anazungumza kuhusu torati na Kristo katika Wagalatia 3:6-29)Na kama hawatamtambua basi wataamshambulia kama msaliti wa mifumo ya Musa yaani Torati. Lakini wale watakaompokea wanakuwa ndio walengwa halisi... Nao watalikuwa ndio wateule wenye kurithi nchi ya kweli ya ahadi, ufalme wa kweli(Yohana 1:11). Wengi walimkataa masiha, na hiyo ikawa ndo laana na mikosi kwa waisraeli hadi hii leo. Waisraeli walivamiwa na kupelekwa uhamishoni nje ya nchi yao ambayo kwa karne nyingi imeshikiliwa na wageni na wavamizi. Miaka mingi imepita lakini bado hakuna amani yerusalemu.

MAFUNDISHO YA YESU:

Kuzaliwa Mara ya Pili na Ufalme wa Mungu

Alipokuwa akihudhuria Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka 30 W.K Yesu alifanya ishara za kustaajabisha, au miujiza. Matokeo ni kwamba, watu wengi wanamwamini. Nikodemo, mshiriki mmoja wa baraza la Sanhedrini, ambayo ilikuwa ni mahakama kuu ya Kiyahudi, anavutiwa na kutaka kujua kujua zaidi kuhusu siri ya miujiza ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kama ishara zile hutoka kwa Mungu. Yesu akajibu na kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa Mungu ( Ufalme wa Mbingu ) pasi kazaliwa mara ya pili. Kwa Maji na Roho... (tazama elementi za kimajia) Pia akamueleza kuhusu siri ya Kristo kuwa mpatanishi wa ulimwengu wa dhambi na Mbingu (Kristo kama Mwana wa Ukweli wa Siri za Juu na Chini). Na kwamba kila ageukia Kristo hatapotea, bali atarithi uzima wa milele ambao ndio asili ya mbingu. Nchi ili hutegemea mbingu, nayo nchi bila Nuru ya mbingu ni upungufu wa utukufu, yaani dhambi ya asili, Anguuko la Edeni. Kristo ni mfano wa ndani wa Nyoka wa shaba wa Musa. Yohana 2:23-3:21; Mathayo 3:16, 17; Hesabu 21:9.

Ufalme wa Mbinguni na Mbegu Haradali.

Akiwa akitembea huko kando ya Bahari ya Galilaya na mara baada ya ktuoka kuwakemea Mafarisayo huko Kapernauni, Yesu anakuta umati wa watu ukikusanyika. Basi akapanda mashua na kuenda mbali kidogo na ufuo, nakuanza kufundisha wale watu kuhusu Ufalme wa Mbingu. Yeye afanya hivyo kupitia kwa mfululizo wa mifano, au vielezi, kila mmoja ukiwa na kikao kinachaofahamiwa na watu.

Na hili ndilo neno lake kuhusu Ufalme wa mbingu unavyonanishwa na mbengu haradali; Ufalme wa Mbingu ni kama punje ya haradali ambayo mtu anapanda. Ingawa hiyo ndiyo mbengu iliyo ndogo sana kati ya mbegu zote, yeye asema, inakuwa na kuwa mboga iliyokuwa kubwa zaidi ya mboga zote. Inakuwa mti ambao ndege wanaende, wakipata makao miongoni mwa matawi yao. Mathayo 13:1-52; Marko 4:1-34; Luka 8:4-18; Zaburi 78:2; Isaya 6:9,10.

Naam na hili ndilo shauri kuhusu chem chem ya uzima. Uzima hutoka katika roho, nayo roho ndiyo neno lenyewe lenye kuishi. Nalo neno lilikuwako, lipo na litakuwapo milele yote. Roho ni mfano wa Jua... Na ni jua katika sura halisi ya ndani. Katika zama zile watu walikuwa hawatambui ya kuwa Jua huwa halizimi moto wake. Hivyo mafundisho mengi ya zama zile yalionekana kuwa ni magumu kukubalika akilini. Na ndio maana mifano na vielezi vilitumika. Nafsi ni kama mwezi. Wenyewe si ile nuru kamili bali ni muakisi wa nuru ya Jua. Mwili ni Dunia yenye kusimama katika msingi wa nuru na giza kwa wakati. Hii ina maana kuwa Roho ndiyo Mpanzi wa kweli naye ndiyo neno lenyewe, nafsi ndio sehemu ya upeo wa mwanadamu wenye kikomo cha kijitambua, na mwili ndio fahamu za msingi za kimwili za mwanadamu yaani kuonja, kuona, kusikia, kugusa na kunusa.

Hivyo shauri mintaarafu dhambi ni hali ya mtu kudumu katika ufahamu wa kinafsi na mwili. Kwani Nafsi ni ile Mbegu isemwayo... Kuona mbegu ni kutojua ya kwamba ndani yake, sura ya mfanyiko mpya umehifadhika. Na ndio kikomo cha upeo wa kuona ki mwili. Vivyo hivyo Ufalme wa Mbingu upo na ndani nje ya kila kitu kilichofanyika, na watu wasitambue. Ili utukufu uliojificha udhihirike basi ni lazima mbegu ife na hivyo mmea kutokeza. Kufa kwa mbegu ni mauti ya nafsi, utukufu wa roho ni ule uzima wa milele ulipo na ndio asili ya yote.

Na hapa ndio kuna fumbo kuhusu Kristo ni nini... Kristo ni ufahamu wenye nuru isiyotoka kwenye vitu vya dunia hii ya maada. Bali yenyewe ni itakayo kwenye utukufu wa Roho. Nafsi Hufa. Roho ni ule uzima, ni lile NENO. Neno kwa maana kwamba lilifanyika na kujidhirisha katika ulimwengu huu wa maada. Ulimwengu huu ni mfano wa utukufu wa mbingu. Uliofinywa katika sura ndogo. Yaonekayo katika ulimwengu huu mdogo, ndiyo yale yale yapatikanayo katika Sura ya Ukumbwa usio na mwisho. Kama ilivyo chini, ndivyo ilivyo Juu.

Kwa shauri hili ndiyo Ukristo ulivyojengwa. Kukombolewa na dhambi ya Asili ili kuuridhi uzima wa kiroho katika Kristo; neno la uzima. Neno la uzima huchukuliwa na wengi kama maandiko lakini kwa kweli si sahihi. Neno la uzima ni Roho yaani Ufalme wa Mbingu, ufalme wa Mpanzi. Yeye Hupanda mbegu chini na hali Mbingu na nchi ni siri moja. Amebarikiwa yule mwenye kutambua Ukweli.

Paulo alijua siri za Kristo kwa upeo wake. Naye huzungumza hivi kuhusu kristo:

1 Wakorinto 2:7-16... Mambo yale yaliyofichika ambayo roho wa mungu humfunulia yeye aliye jiandaa kupokea shauri la kweli yaani utambuzi sahihi/maarifa ya kweli ya mbigu.

Tufute yote!

hariri

Yaliyomo ya makala hayalingani na masharti ya kamusi elezo. Kuna ukurasa ndefu lakini habari zilizomo hazikupangwa kwa namna inayoeleweka.

Makala inatakiwa kueleza: Wakristo ni akina nani, idadi na namba/takwimu, muhtasari ya chanzo, madhehebu (orthodoksi- katoliki- protestant- pentekoste), mafundisho na mielekeo, uhusiano na imani kama Uyahudi na Uislamu, upinzani dhidi ya Ukristo katika falsafa n.k. ... . Sioni kitu kama hiki. Kama hakuna mwenye ushauri jinsi gani kupeleka makala pale panapotakiwa tufute kwanza yote na tuanze upya. Vilevile ukurasa huu wa majadiliano. Sioni mapendekezo wala maoni yanayosaidia kupanga makala. Musa alisema ya kwamba anaendelea kushughulika. Kweli kuna mamabo kadhaa yanayoweza kufaa lakini kwa ujumla bado sijatambua muundo utakaosaidia. Mnasemaje? --Kipala 13:50, 3 Juni 2007 (UTC)Reply

Subira

hariri

subira subira kipala! nadhani kamusi ilezi si jukwaa la kutengeneza habari za utafiti ki habari tu... Tunaweza kujadili mambo kwa nyuma ili ku adapt theme kwenye kurasa ya mbele. Na hasa hasa mambo ya metaphysics na falsafa hutatuliwa na Mitazamo na thesis. Kwa kweli si mlengo wa habari tu. Nia ni kujaribu ku post muhtasari wa Ukristo, Kanisa, mamlaka yake, chimbuko na labda wengine mnapenda mkururo wa kihistoria. Sawa? Bado kazi inaendelea... Makala ya mbele inahitaji kubadilishwa kwa ujumla. Halafu niulize kitu kimoja labda: kwani ni nini maaana ya kujadili kutokana na makala ya mbele? ;)

Nita jaribu makala za kisayansi/fizikia pia siku zijazo nadhani mwelekeo utakuwa tofauti na hapa :)

Haya Twende !

hariri

naleta pendekezo sasa:

mbele kuwa na (1)Aya ya kwanza (ukristo) (2)Kuhusu Masiya (3)Link kuelekea habari za Musa (4)Link kuelekea habari za Yesu (5)Mafundisho ya Yesu (6)Kanisa lilikotoka(Itahitaji habari zaidi) (7)Kanisa leo Nitachangia zaidi na kutengenza makala nyingine kuhusu unajimu, majia, gnosia na mengineyo. Lakini mpaka hapo naona msingi umeonekana Naam, mnasemaje wenzangu?

Nakushukuru kwa bidii zako za kupanua makala hii. Hata hivyo nakosa marejeo. Kamusi elezo isitoe maoni ya mtu binafsi bali habari zilizokubalika na wataalamu wengi. Ndiyo sababu ni muhimu kurejea habari za makala na vitabu vinavyolithibitisha uliloandika. Naomba utuelekeze kwa marejeo yanayofaa. Asante! --Oliver Stegen 11:56, 13 Juni 2007 (UTC)Reply


Naam Oliver, hapa naona natumia zaidi kitabu hiki kiitwacho Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi, Halafu kuna Hii Biblia yenye itifaki: Biblia Takatifu toleo la 'jimbo la Bologna'. Na tafsiri ya ya zamani ya biblia.
kingine ambacho nakifanya ili kuepeka mlengo binafsi ni kuweka maneno toka kwenye biblia moja kwa moja na kusemea jambo. Hii inafanya makala kuwa ndefu lakini sina jinsi. Kinachotakiwa mtu aone maana.
Nakuhaikikishia kuna mfuatano sahili wa kauli, vifungu na mawazo. Na kama unafuatilia kwa makini; hii ndio nafasi ya kukosoa. Tafadhali kila unapona kama wazo binafsi... bandika hoja hapa ili makala ishughulikiwe. Ahsante :)
Pia nitahitaji ufundi wa kuweka marejeo kwa kila neno lenye kuhitaji!

Kazi inaendelea !

Ninajitahidi kuipata makala sura thabiti hata kwa mtu yeyote ambaye anataka kuchunguza mapokeo na falsafa ya ndani ya Ukristo... Kuna vingi siwezi kusema moja kwa moja lakini kwa ufundi wa kutumia masimulizi ya kihistoria, ninatumaini itawezekana kubainisha, kwa jinsi yake. Maana mie pia ni mchunguzi tu, nasi muumini.

mpaka kwenye kanisa la kati, nimekuwa nikirejea kwenye biblia yenyewe zaidi... Naona sasa naingia kwenye historia sasa :( ... Nakaribisha yeyote ambaye anaweza kusaidia maneno machache, tusaidiane kuhariri pia :)

Kanisa Leo ninatazamia iwe na sura mulikaji juu ya hali ya sasa kutokana na mchetuzi wa Asili ya Ukristo, si tu kwa nje; aghalabu na dhamira zake pia zimulikwe na ndio sababu kwanini niliona ulazima wa kuchimba Ukristo kwa ndani pia.

Tofauti ya msingi wa makala za habari na zile za dini ama falsafa; ni katika kugusa kiini cha chimbuko ki roho... Mtu akikwepa tu hiko kiini. Basi mashauri yote yanabakia kuwa kama 'red herrings', jambo ambalo linaleta mianya ya tetesi na masimulizi kihistoria yasiyo ulazima (Kama si chakula cha mawazo tu) na hata uzushi usio na maana ya kimsingi na migongano wa kiitikadi na dhana.

Basi tuwe makini na historia za kweli kabisa na tunachokielewa juu ya hicho...

Ahsante !--Moses 07:54, 24 Juni 2007 (UTC)Reply

Mpangilio

hariri

Mose umekuwa mchapa kazi kweli. Pole na kazi na hongera ya jitihada! Ila tu naona makala jinsi ilivyokua itahitaji uhariri. Sababu moja ni itakuwa makala ndefu mno. Nikona mpangilio wako umeingia sasa sana katika historia ya kanisa. Naona itakuwa lazima kuiasua na kupanga makala za pekee. Kuhusu makala yyenyewe naona sawa ukiendelea lakini itahitaji uhariri ili tufike kwenye kiwango cha kamusi elezo. --Kipala 13:02, 24 Juni 2007 (UTC)Reply

Sawa kipala... Tupo pamoja !--Moses 15:41, 24 Juni 2007 (UTC)Reply

Makala hii ya sasa

hariri

Nimepitia ukurasa huu leo na kukuta masahihisho mengi ambayo nadhani hayapendezi hasa kuwa jarida la watu wote kusoma na

kupokea hivyo na changamoto ya mjadala.

Ukristu ni dini kuu ya ulimwengu, ikiwa na wafuasi zaidi ya bilioni mbili (taz. Dini); kitabu chake kitakatifu kinajulikana

kama Biblia.

-Kuusema ukristu kwa msingi wa ufafanuzi wa takwimu za idadi ya waumini na kuuita ni dini kuu hakusaidii kumfanya mdadisi

aelewe ukristo ni nini. Kwa kweli takwimu zina sehemu yake. Lakini katika mfumo huu mpya wa jukwaa la maarifa vijana na

watoto wetu wanapenda kujua kinaga ubaga kuhusu dini mbali mbali na hivyo ni vema tukaweka habari za kiufundi za kiuchunguzi

ili kusaidia ufahamu na maarifa ya kizazi chetu na kijacho wanaofanya chaguo sahihi la kujitambua kwa chocote kile

wanachojisikia kwa wakati kuhusiana nacho. Jukwaa hili lijitahidi kuepuka mlengo wa kuuza picha ya mtu aliye ndani(mwenye

maslahi na hoja); ni vema kila mchangiaji ajipime ikiwa anachangia toka nje ama ndani. Ikiwa yuko ndani basi awe tayari

kukosolewa na aliye nje. Lakini mchangiaji bora kabisa ni yule mwenye kuona ndani na lakini akasema toka nje na ingawaje

anauelewa mpana na hata zaidi ya somo lenyewe. Hii italeta mseto bora ambao ndio hasa; makala ambazo watu wa leo na wale

waliokatika kusaka zaidi hutafuta.

yaani Mpakwamafuta (Kristo kwa Kigiriki),

-Kristo husemwa pia kuwa ni mpaka mafuta, lakini hili ni swala mjadala katika jukwaa la teolojia. Maana kuna mengi sana humo.

Lakini ieleweke kuwa teolojia zote zina mapengo yake. Na baadhi ya hayo mapengo yanaweza kutafutiwa majawabu tokea kwenye

vyanzo mbalimbali, hata hapa kwenye wikipedia; ni uwanja mmoja mmojawapo ambao wengine wapo tayari kutoka huo mchango. Kwa

mfano, neno mesiya lina mizizi sawa na neno 'mashaikh' la kiebrania kuwa na maana ya mwenyekutwaa watu(kitu) toka kwenye

vingi... Sasa aliyetoa neno kristu toka kwenye kigiriki afanye utafiti zaidi atakuta na hili. Ndio maana kabla makala hii

haijaandikwa hivi. Mesiya ilifafanuliwa kimkato na neno Mkombozi.

Musa, mwanamapunduzi aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu

-Musa alikuwa ni mwanamatengenezo(Social Reformer, samahani kuleta lugha ya kigeni), mapinduzi yana sura ya kupindua madaraka

na kuinua mapya na pia kubadili mifumo ya kijamii... Musa alikomboa na kujaribu kusimamisha upya msingi ya kijamii kwa

Torati. Na hivyo haya ni matengenezo ambayo ni tafsiri sanifu ya neno reformations(tena, samahani)


Maana Ya Kristo,

-Aya zote zilizo chini kichwa hichi cha habari hazitoshelezi kufafanua:- Ifahamike kuwa sisi wote tupo katika kujifunza na

kuongeza nuru yetu katika kuyajua na kuyafahamu mambo yahusiyo Ukristo; hivyo kristo kama neno ama hali ni vema kufafanuliwa

ili kuwa mtu yeyote; hata ambaye hajapata kusikia kuhusu ukristo aweza kusoma na kupata picha halisi. Sasa aya yote iliyobaki

pale chini huzungumza juu ya 'mystical knowing'(Kujua kwa jinsi ya ndani, jinsi ya kiroho). Na katika hili ifahamike kwamba

Imani ni kuwa na Hakika. Mafundisho yote ya nje ya dini kulenga katika kumuongoza mwenye kuanza kwa kusadiki afike mahala,

roho yake itaanzamfunza na kumjenga na kuwa taa yake. Mwongozo huu wa kiimani ni 'kernel' ya dini zote; na ndiyo chenye

kuitwa IMANI hasa. Hiyo dini ni mafundisho ya nje ya mwongozo; pia kusema mapokeo(mfano wa palilizi). Lakini Imani ndiyo

tunda lenyewe. Kuna ufundi ambao dini zote zaweza kuelezwa kufika katika shina hili lenye kuunganisha lugha ya nje iliyopo

katika dini zote na Kilicho hasa hasa katika undani wa mtu. Na jukwaa hili la wikipedia ni uwanja wetu wa kufanya hili

kuwezekana. Inawezekana kabisa mtu hajawahi kabisa kudhania hili, lakini ni hivyo. Kilicho muhimu ni watu kuwa nia moja

kusaidia kushiriki upeo wa kuona na kuwakilisha.

Mafarakano Makuu Kati ya Wakristo

-Badala ya kuelezea ya mafarakano; ni bora zaidi kueleza kilicho kiini halafu kumulika ni jinsi gani vingine huchipukia. Ndio

maana makala ya mwanzo ililenga kueleza kiini. Historia ni mchakato wa nje katika nyakati. Ina sehemu yake. Lakini zama hizi

kuna uwezekano kabisa kutenganisha Historia na sayansi ya metamofosia ya kiroho ambayo dini zote hunyooshea kidole. Na hapa

kwenye hili jukwaa ni ukumbi mmoja wapo wa kufafanua hivi vyote viwili na hata kuvibainisha. Ingelikuwa ni bora makala zote

za dini ziwe sura mbili zenye kuchambuliwa moja ni ya kihistoria na ingine ni kuchambuliwa kwa kiini cha uasili

mbegu(essence) cha mafundisho yake kwa msaada wa moja kwa moja wa yale yalisemwa katika maandiko yake ili kuunganisha Mtu na

Manani(The Divine). Nalo hili lawezekana kabisa.

Utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia mwanamke "uzao wako utamponda kichwa" nyoka,

yaani shetani

-Katika maandiko ya dini mbali mbali kuna visa vya masimulizi vyenye kubeba mafumbo ya kiroho(Allegories) ambayo ni vema

kutochukuliwa kijuu juu tu kwani mengi ya hayo hupwaya katika mizani ya sura halisi ya mambo. Hii ndiyo yenye kuleta hali ya

wengi kupuuzia mafundisho ya dini mbali mbali na kuyaona ni upuuzi ama mambo magumu kueleweka kwa mtu wa kawaida. Basi ni

vema kutoka michango yenye mantiki iliyowekwa wazi kumulika dhana maelezo. Na vile vile ni jukumu la kila mtu kusahihisha ama

kukosoa pale ambapo mwingine anaonekana kama kwamba anaichukulia mifano kama hiyo kwa juu juu. Na pia kutafuta michango zaidi

kuboresha picha.

Naomba kuwakilisha hoja.

Ni hayo tu

mengine yatafuatia baadaye

--Moses (majadiliano) 17:21, 26 Aprili 2008 (UTC)Reply

Rudi kwenye ukurasa wa " Ukristo ".