Majadiliano:Vielezi
Vielezi ni maneno yanayoelezea tendo lilivyofanyika au litakavyofanyika.Vielezi hufafanua kitendo kilitendeka wapi,vipi,mara ngapi na namna gani.
Aina za vielezi
haririKuna aina nne 4 za vielezi.aina hizo ni:
- (i)Vielezi vya namna au jinsi
- (ii)Vielezi vya mahali
- (iii)Vielezi vya idadi
- (iv)Vielezi vya wakati
(i)Vielezi vya namna au jinsi
haririNi aina ya vielezi ambavyo huelezea namna au jinsi ya kutendeka kwa tendo. Vielezi hivi huelezea jinsi gani tendo hilo limetendeka.
(ii)Vielezi vya mahali
haririNi aina ya vielezi ambavyo huelezea mahali kulikotendeka tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka wapi.
(iii)Vielezi vya idadi
haririNi aina ya vielezi ambavyo huelezea idadi ya kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka mara ngapi.
(iv)Vielezi vya wakati
haririni aina ya vielezi ambavyo hueleza wakati wa kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza ni lini hasa tendo hili limetendeka.