Majadiliano:Waridi

Elimu ni ni zaidi ya kusoma. Aliyeelimika ni mnyenyekevu lakini msomi ni mwenye majivuno. Aliyeelimika ni msikivu bali aliyesoma ni mropokaji. Aidha aliyeelimika anatii ila aliyesoma ni mbishi kwa sababu hufikiri anajua kila kitu. Pia aliyeelimika ana heshima lakini aliyesoma ana dharau. Ndugu yangu, jiulize wewe ni nani? Ni msomi au umeelimika? unatumiaje elimu yako katika jamii inayokuzunguka?

Aliyeelimika anatumikia, anasaidia, ananyenyekea, anatii na daima anakubalika na wote katika jamii. Ewe kijana, kumbuka kuwa wewe ni mzazi na mlezi wa kesho. Sasa kama mpaka sasa haujaelimika wala hauna mpango wa kuelimika unategemea kauandaa familia, jamii na taifa la aina gani pale ambapo utashika nafasi yako kama mzazi, mlezi, kiongozi na mwalimu wa jamii? Utaweza kweli kubeba majukumu yako kwa uaminifu ikiwa wewe mwenyewe mpaka sasa hali yako ni mbaya? JITAFAKARI SANA.

Rudi kwenye ukurasa wa " Waridi ".