Majadiliano ya Wikipedia:Kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili

Ombi la maoni yako kuhusu kuunda Mfumo wa Usajili kwa ajili ya Matukio

hariri

Habari ndugu Mwanawikimedia,

Ninawandikia nikiwa kama Balozi wa Bidhaa kwa Jamii ya Waswahili kwaniaba ya Timu ya Kampeni katika Shirika la Wikimedia Foundation. Timu ya Kampeni ya Shirika la Wikimedia Foundation inajikita kujenga na kuboresha zana kwa ajili ya waandaaji na washiriki wa kampeni. Tunataka kuhakikisha kuwa ni rahisi kwa kila mtu kuandaa kampeni, kama vile miradi ya Wiki Loves Africa, Wiki Loves Earth, Wiki Loves Women n.k. na kwamba iwe ni rahisi kwa washirki kufurahia na kuridhika na kampeni hizi kama washiriki.Tutakuwa tukifanya mabadiliko kadhaa, na tungependa kusikia maoni yako!

Mradi wa kwanza: Usajili wa tukio: Kwa sasa tunashughulikia kuunda mfumo wa usajili wa tukio, ili uweze kuwasajili washiriki wa tukio husika kwa urahisi kwenye kurasa za tukio za wiki. Mfumo huu ungeunganishwa na Dashibodi ya Programu na Matukio. angalia ukurasa wa mradi na karibu utushirikishe maoni yako kwenye ukurasa wa majadiliano. Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu na kwenye mradi huu, na timu yetu inapenda sana kusikia kutoka kwako.

Unaweza kuwasiliana na Balozi wa Bidhaa kwa Jumuiya ya Waswahili Ndg: Antoni Mtavangu (amtavangu-ctr@wikimedia.org) kwa taarifa zaidi kupitia lugha yako ya Kiswahili na pia kwa lugha ya Kiingereza.

Pia, kama ungependa kujifunza zaidi kuhusu timu yetu na miradi yake, basi tafadhali jiandikishe ili kupata majarida yetu!

Asante!
Antoni Mtavangu (kwaniaba ya)
Timu ya Kampeni, Wikimedia Foundation

Rudi kwenye ukurasa wa mradi " Kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili ".