Majadiliano ya Wikipedia:Mwongozo

Latest comment: miaka 14 iliyopita by Kipala

eti jina liwe "ukufunzi" au heri mwongozo ? --Kipala (majadiliano) 15:55, 1 Desemba 2009 (UTC)Reply

Nimetafsiri kadiri kamusi ya TUKI inavyosema. Ukiona si sawa, basi endelea!--Muddyb MwanaharakatiLonga 17:01, 1 Desemba 2009 (UTC)Reply
Nisipokosei Kiing. "tutorial" inaweza kuwa na maana kadhaa. Neno la TUKI inamaanisha aina ya semina kwenye chuo kikuu (nisipokosei). Ila tu je itaeleweka nje ya wanafunzi? Wewe unaonaje "Mwongozo" - je haieleweki kirahisi zaidi? Kama la, tuache. Kama ndiyo: Tuhamishe. --Kipala (majadiliano) 10:03, 2 Desemba 2009 (UTC)Reply

(Yafuatayo yamehamishwa kutoka Majadiliano ya mtumiaji:Muddyb Blast Producer
:Pole mzee Kipala. Dhahili kamusi yako labda ya kitambo! Tazama hii:

tutor n 1 (at colleges, etc) mkufunzi. 2 mdarisi, mwalimu binafsi. 3 (GB) mwalimu wa chuo kikuu, mhadhiri. vt 1 fundisha, funda; darisi. 2 jizoeza, dhibiti, chunga. ~ial adj -a ukufunzi. n semina ya ukufunzi.


Basi hapo ndipo nilipoipata! Hata Wikipedia ya Kiingereza inayo kurasa ya mwongozo (guideline) na hii ya "tutorial-ukufunzi". Kama nilivyosema. Ukiona siyo, basi endelea!--Muddyb MwanaharakatiLonga 11:16, 2 Desemba 2009 (UTC)Reply

Kamusi yangu ileile. Hapa naona: ni maana ya pekee (kawaida kabisa kila neno kuwa na maana mbalimbali ukitafsiri). Nashauri hapo acha kamusi kando - je wewe mwenyewe unaonaje? Neno gani linasaidia hasa? (Jaribu kukumbuka ulionaje ulipoanza wikipedia). --Kipala (majadiliano) 12:28, 2 Desemba 2009 (UTC)Reply
Sawa. Hamisha tu. Lakini usisahau kama kuna "vikurasa" au "subpages" ambazo zinatumia jina la "ukufunzi"! Endelea tu. Pia, wakati nilivyojiunga, kwangu ilikuwa rahisi kwa sababu nilikuwa ninajua kutumia HTML code kiasa - na vilevile nilikuwa nina nia ya kuweza kutumia na kuchangia Wikipedia. Sijui wao. Labda wapo kwa ajili ya Laptop na zawadi nyinginezo (mzaha!) Basi we endelea tu mzee wangu.--Muddyb MwanaharakatiLonga 13:06, 2 Desemba 2009 (UTC)Reply


Hongera mzee Kipala, kwa anzisho la "muundo". Nilishaanza kutoa macho baada ya kusoma yale yaliyomo kwenye ukurasa ule - kule kwenye Wikipedia ya Kiingereza! Haya, tuendelee!--Muddyb MwanaharakatiLonga 13:33, 2 Desemba 2009 (UTC)Reply

Sasa naona mambo yashakuwa mazuri. Hongera kwa kazi ya kutengeneza mwongozo huu. Kila la kheri.--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:16, 8 Desemba 2009 (UTC)Reply
NAomba jaribiha hasa hii: Wikipedia:Jedwali. Je inaeleweka? Sijasahau kitu? --Kipala (majadiliano) 13:56, 8 Desemba 2009 (UTC)Reply
Return to the project page "Mwongozo".