Majadiliano ya faili:Pemba-Wete.PNG

Latest comment: miaka 15 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Kuna bwana nimeona maelezo yake akisisitiza juu ya uwekaji wa Laiseni katika picha. Ni muhimu sana na ninakumbuka ulikuwa ukisisitiza juu ya matumizi ya laiseni katika picha. Utata utakuja tu, kwa kuwa jamaa keshaanza balaa hilo! Angalia hapa. Tufanye mpango wa kuziunda mabano yote ya laiseni. Unaonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 07:19, 15 Septemba 2008 (UTC)Reply

Picha hii ina maelezo kuwa ni kutoka commons; ninachofanya mara nyingi ni kuchukua picha kutoka commons au wiki nyingine na kiuibadilisha kidogo, kwa mfano hapa kuongeza duara nyekundu kwa kuonyesha mahali pa Wete. Kwa mabadiliko madogo ya aina hii hasa kama ni kubadilisha maandiko au jina la mahali kwa umbo la Kiswahili - hatuna haja kubwa ya kuongeza maelezo mengi. Labda temnpleti ndogo "Picha ya commons iliyobadilishwa kidogo"? --Kipala (majadiliano) 13:59, 15 Septemba 2008 (UTC)Reply

Haijalishi umebadilisha kidogo sana. Wao inaonyesha wanataka License Tag, kama jinsi ilivyo katika Wikipedia zingine! Kwani hata kule de, simple, en, es n.k. Wao huwa wanaweka License Tag katika kila picha ionekanayo katika Wiki zao! Mengineyo: Hata kama tutakitangazo kidogo, nacho kitafaa. Cha muhimu ni kujua kama ile picha ni ya GFDL? Ikiwa sawa, basi wekea laiseni ikiambatana na kiungo kutoka katika Wiki iliyotokea. Au waonaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 14:09, 15 Septemba 2008 (UTC)Reply
Return to the file "Pemba-Wete.PNG".