Majadiliano ya jamii:Shule ya Upili
Latest comment: miaka 14 iliyopita by Baba Tabita
Sijawahi kusikia "shule ya upili". Je, siyo "shule ya sekondari"? Tuache kutafsiri sisisi (yaani neno kwa neno); mara nyingi ni utafsiri wa uwongo wala Kiswahili sanifu. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 13:45, 16 Desemba 2009 (UTC)
- Ninakubali jamii iwe "shule ya sekondari". Hata hivyo "shule ya upili" husikika Kenya mara nyingi nadhani ni mapokeo ya mahali. Ukienda Zanzobar utapata "Skuli ya sekondari" (kama lugha rasmi!). Google search:
- Shule ya sekondari + 393.000
- Shule ya upili: 19.600 (kama Wakenya wangetumia zaidi Kiswahili mtandaoni idadi ingekuwa kubwa kiasi, nadhani)
- Skuli ya sekondari: 473
- Skuli ya upili: 2
- Pendekezo: makala yenye jina la "Shule ya Upili ya Alliance" n.k. zikae lakini zipate redirect "Shule ya Sekondari ya Alliance"; jamii iwe Shule ya Sekondari