Majadiliano ya kigezo:Sanduku la habari za nchi

Latest comment: miaka 18 iliyopita by Kipala in topic Pendekezo:

Pendekezo: hariri

A) "Mji mkubwa kushinda miji mingine yote" iwe "mji mkubwa" -itatosha na kueleweka

B) "Kodi ya simu" - "Kodi" hakika si Kiswahili - nimesahau neno sanifu najaribu kuipata kutoka Bongo

C) "Intaneti TLD" - "Herufi za Kikoa" twende kwa orodha la http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/sw_TZ_glossary_klnX_1.html hawana "TLD" lakini maana yake ni herufi za kikoa cha mwisho au cha juu zinazoonekana kwenye anwani za wavu za nchi fulani.

D) "Msongamano wa watu" - nimetumia "wakazi kwa km²"; msongamano ni pendekezo la kamusi lakini kwangu ina herufu ya "kubana,kubanana"- "wakazi kwa km²" inaweza kueleweka vizuri na rahisi zaidi...


Ninakiri ya kwamba sina uhakika jinsi gani kutumia hiki kielelezo. Matt, unaweza kutoa maelezo kidogo? Kuandika nini wapi?? NB: "Template" ni kielelezo au kiolezo (ingawa orodha ya kilinux inataja "templeti") --Kipala 19:33, 21 Aprili 2006 (UTC)Reply

Return to "Sanduku la habari za nchi" page.