Amina
Amina, salam! Ninashuku kwa pole yako! Pia, ninajitahidi niweze kusahau mwendendo wa tabia zetu tulizokuwa nazo hapo awali ili nisiumie zaidi! Basi kila la kheri huko ulipo! Wako kijana mtiifu,--Mwanaharakati (Longa) 05:37, 9 Machi 2009 (UTC)
- Dada Amina, salam. Khe! Bado unanishangaza kidogo. Kiswahili umejifunza ukiwa Ulaya ama Afrika? Maana unajua Kiswahili kizuri! Hebu nipe siri ya Kiswahili chako!!!!!!!! Ni yuleyule kijana wa DSM, TZ, Muddyb,--Mwanaharakati (Longa) 10:22, 23 Machi 2009 (UTC)
- Alaa, kumbe!! Haya, natuma ya kwamba umeona kila mtumiaji amejielezea kiwango cha lugha anazojua! Pia, ningependa kuona nawe uwe mmoja kati ya walionyesha uwezo wao lugha katika kurasa za mtumiaji! Tazama hii. Halafu mfano huu:
Wikipedia:Babel | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Hilo jedwani unaliona linatakiwa liwe katika ukurasa wa mtumiaji. Unaliweka kabisa ya ukurasa wako! Je, ni lugha ngapi unazungumza? Ikizitaja, labda nitaweza kukusaidia kuliwekea katika ukurasa wako wa mtumiaji! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 04:55, 12 Juni 2009 (UTC)
- Basi tayari nimeshaweka kama jinsi ulivyoomba!!! Kiingereza nimeweka sehemu ya 4. Kiswahili sehemu ya 2 na Kiswidi ni sehemu ya... ya mama!! Kila la kheri, dada. Wako mdogo mtiifu,Muddybau,--Mwanaharakati (Longa) 12:37, 24 Juni 2009 (UTC)
mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu
haririAmina, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Ukihitaji msaada wangu upande wa kumwandikia, karibu unijulishe. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu,
--Baba Tabita (majadiliano) 08:12, 10 Oktoba 2009 (UTC)
Picha yako!
haririSalam, dada Amina! Nimeshaweka picha yako kwenye ukurasa wako wa mtumiaji tayari. Ukiwa una-lingine, basi usisite kuniuliza, dada mpendwa! Salam tele kutoka mjini Buguruni, Ilala, Dar es Salaam, Tanzania! Wako,--MwanaharakatiLonga 06:27, 3 Mei 2010 (UTC)