Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Michango yako hariri

Ndugu, pamoja na kukukaribisha naona tunahitaji kuwasiliana. Umeanzisha makala technology na Mechanics. "Technology" nilipaswa kufuta matini na kuweka kielekezo badala ya matini yako. Sababu ni hizo: 1) umetumia jina lisilo Kiswahili ilhali hapa tuko kwenye Wikipedia ya Kiswahili na mambo unayotaja kuna istilahi za Kiswahili. 2) mada hiyo ina makala tayari (tekinolojia), 3) ulileta maelezo bila kuonyesha chanzo au uthibitisho wowote, pamoja na maelezo finyu. Tafadhali tumia muda kusoma Wikipedia:Mwongozo. Angalia Mwongozo kuhusu Vyanzo. 4) Kuhusu Filamu "Mechanics" nimeiweka kwenye orodha ya ufutaji, maana huelezi kitu tena huonyehsi vyanzo. Pia umejaribu kuingia picha kutoka google ambayo ni marufuku hapa. Soma Mwogozo kuhusu picha. Una muda wiki 1 hivi kuisahihisha ukipenda. Baadaye itafutwa. 5) Halafu naomba sana uitikie na kuthibitisha hapa kwamba umesoma maelezo yangu.Naona wewe u mgeni nadhani huna nia mbaya. Ili tuweze kushirikiana tafadhali uandike hapo chini kwamba umeelewa, menginevyo inaweza kutokea kwamba utazuiliwa kuingia. Kipala (majadiliano) 18:22, 23 Mei 2021 (UTC)Reply