Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Justine Msechu (majadiliano) 16:46, 12 Oktoba 2024 (UTC)Reply

Ndugu, una juhudi kweli, lakini legeza mwendo: tafadhali, tengeneza makala za maana zaidi na zisiwe fupi kama hizo zako za mwisho. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:57, 13 Novemba 2024 (UTC)Reply

Kwa kuwa husikii, nimekuzuia kwanza kwa siku 1. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:08, 14 Novemba 2024 (UTC)Reply
Karibu tena katika uhariri, ila naona makala ya leo si tofauti na zile zilizotangulia. Afadhali uchague aina moja ya makala, kwa mfano miji ya nchi fulani na utunge makala zinazofanana. Kubadilibadili mada kunafanya kazi yako na yetu iwe ngumu zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:46, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
sawa sawa nitafanya hivyo Mike dani (majadiliano) 10:02, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
Lakini pia , naona miji mingi ninayopata Ina taarifa fupi sana, hazina taarifa ndefu Mike dani (majadiliano) 10:12, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
Ni kwa sababu unaandika juu ya miji yenye wakazi 15-100 tu!!! Ni mitaa. Tafsiri makala juu ya miji mikubwa na habari zitakuwa nyingi. Lakini kwanza andika kurasa fupi zenye muundo uleule, ila sahihi. Utatupunguzia kazi ya kufanya marekebisho mengi mno! Ukipenda nitakuandalia sampuli. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:30, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
ningependa kupata sampuli Mike dani (majadiliano) 10:47, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
Tumia kama sampuli [[Ezhou]]. Ni sahili sana na inatosha kwanza. Sanasana kazi ni kubadilisha majina, idadi ya wakazi n.k. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:51, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
sawa sawa kwahiyo inabidi niandike nakala za miji mikubwa , lakini kwanza niandike kurasa fupi Kwa usahihi sio lazima nakala nzima Mike dani (majadiliano) 12:41, 18 Novemba 2024 (UTC)Reply
Ndugu, unazidi kuchanganya: kuna Kitwe Tanzania na Kitwe Zambia. Pia ukurasa kuhusu Sokodé ulikuwa ukiwa na jina bila mkazo juu ya herufi ya mwisho...
Habari ndugu @Mike dani Naomba uzingatie uandishi sahihi wa makala za wikipedia
1: Makala inatakiwa iwe na vyanzo vya kutosha (external and internal link) ili kumsaidia msomaji kuelewa habari kiundani
2: Makala za wikipedia zina muundo maalumu au mpangilio maalumu. Nasisitiza kuelewa kwanza namna ya kuunda makala kabla ya kuanza kuunda makala na kuchapisha, Hivyo pitia makala zako zote na urekebishe Justine Msechu (majadiliano) 08:44, 21 Novemba 2024 (UTC)Reply
sawa sawa nazirekebisha Mike dani (majadiliano) 08:47, 21 Novemba 2024 (UTC)Reply