Nako 2 Nako karibu sana kwenye wikipedia ya Kiswahili! Nafurahi ya kwamba safari hii watu wa bongo wameamka kidogo. NAtumaini ya kwamba utaendelea!

Halafu ombi: nashukuru ukijitahidi kukaza kidogo staili ya makala zako. Bongo Flavour na Inspector Haroun niempenda na kuelewa vizuri.

"Hip Hop ya Bongo" ni mfano wa makala inayofaa kuhaririwa. Sentensi kama "sizani kama kuna mtu ambaye hafahamu Hip Hop ya Bongo, hivi Karibuni kulikuwa na Malumbano yasikuwa na msingi mengi sana kivipi?". Mambo matatu: a) lugha kama "sidhani" haifai katika kamusi elezo; b) bila shaki ni wengi ambao hawajui Hihop ya Bongo; kumbuka wazee au Wakenya au watu huko Kisangani au kote duniani. c) habari za "malumbano" hazina maana; ama ni muhimu ya kutohsa ili ueleze ni nini au tuiache. Asante --Kipala 13:29, 23 Agosti 2007 (UTC)Reply