Makamu wa askofu
Makamu wa askofu ni cheo cha Kanisa Katoliki anachopewa askofu au padri ili kutimiza baadhi ya majukumu ya askofu wa jimbo na kwa niaba yake.
Katika Mkusanyo wa sheria za Kanisa la Kilatini kanuni 475 inaagiza: Katika kila jimbo askofu wa jimbo anatakiwa kumteua makamu wake ili, kwa kutumia mamlaka ya kudumu aliyonayo kufuatana na kanuni zinazofuata, amsaidie askofu mwenyewe katika kuongoza jimbo zima".
Mbali na huyo, anayehusika na jimbo lote na masuala yote, askofu anaweza kumteua makamu mwingine au zaidi kwa sehemu maalumu tu ya eneo la jimbo au ya uchungaji wake.