Makongoro ya ng'ombe

Makongoro ya ng'ombe ni miguu ya ng'ombe. Vipande vyake vinatumika katika chakula sehemu mbalimbali duniani, sanasana kwenye mapishi ya Asia, Afrika, Ufaransa na huko Karibi.[1] Mapishi ya Kilatino pia hutumia makongoro ya ng'ombe kwenye mapishi ya asili.

Ukiachana na ng'ombe, makongoro ya wanyama kama mbuzi, kondoo na nguruwe yanaweza liwa na kutumika kwenye chakula na mapishi ya kiasili.

Marejeo hariri

  1. Williams, Hazelann (2012-10-02), "Sole food: the eating of feet", The Guardian (kwa en-GB), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2023-05-14