Makumbusho ya Kitale

Makumbusho ya Kitale yanapatikana magharibi mwa Kenya, kilomita 380 kutoka mji mkuu wa Nairobi, na kilomita moja kutoka mjini Kitale.[1]. Ni makumbusho ya kwanza ya nyumbani nchini Kenya yaliyofunguliwa mwaka 1924.

Mwanzo makumbusho hayo yalikuwa yakijulikana kama The Stoneham Museum,[1] likiwa na jina la Colonel Hugh Stoneham aliyekuwa akikusanya vitu vya sanaa katika jumba hilo hadi alipofariki dunia mwaka 1966.

Baadaye mwaka 1974 makumbusho hayo yalifanywa kuwa makumbusho ya kitaifa na kuitwa Makumbusho ya Kitale.[2]

Bango la makumbusho ya Kitale au Makumbusho ya Kenya magharibi.

Vitu vingi katika makumbusho hayo vimechukuliwa kutoka katika jamii za makabila mbalimbali ya Kenya, yakiwemo ya Waluyha, Wamaasai na Waturkana.[2] Makumbusho hayo yanaonyesha utamaduni halisi wa Wakenya, silaha walizotumia, vyombo vya kupikia, na ala za muziki.[2] Pia baadhi ya wanyama kama mamba, kobe na aina nyingi za nyoka hupatikana katika makumbusho hayo.[2]

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 National Museums of Kenya - Kitale. Museums.or.ke. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-11-11. Iliwekwa mnamo 2014-08-18.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Department Of Information » Kitale Museum. Kenyanewsagency.go.ke. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2014-08-18.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makumbusho ya Kitale kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.