Malengo endelevu

Michael Octavian Mwananzila

Malengo Endelevu (kwa Kiingereza: Sustainable Development Goals, kifupi: SDGs) ni mkusanyo wa malengo 17 yalopangiliwa kwa faida ya watu wote.[1]

Vijana wa Peru wakiwa wameshika mabango ya Malengo Endelevu.

Malengo endelevu yalianzishwa mwaka 2015 na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa likiwa na malengo ya kufikiwa mwaka 2030, kama sehemu za ajenda za mwaka 2030.[2][3][4]

Malengo endelevu ni:

  1. Kutokomeza Umaskini
  2. Kukomesha Njaa
  3. Afya Njema na Ustawi
  4. Elimu Bora
  5. Usawa wa Kijinsia
  6. Maji Salama na Usafi
  7. Nishati Mbadala na Gharama Nafuu
  8. Kazi Zenye Staha na Ukuaji
  9. Viwanda Ubunifu na Miundo Mbinu
  10. Kupunguza Tofauti
  11. Miji na Jamii Endelevu
  12. Matumizi Uzalishaji Wenye Uwajibikaji
  13. Kuchukua Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi
  14. Kuendeleza Uhai katika Maji
  15. Kulinda Uhai katika Ardhi
  16. Amani Haki na Taasisi Madhubuti
  17. Ushirikiano katika Kufanikisha Malengo

Marejeo

  1. dpicampaigns. "About the Sustainable Development Goals". United Nations Sustainable Development (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-11-09.
  2. "United Nations Official Document". www.un.org.
  3. "Transforming our world: the 2030 Agenda for Sustainable Development". United Nations – Sustainable Development knowledge platform. Iliwekwa mnamo 23 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Global Goals | Policy and advocacy". Sightsavers (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2017-09-25. Iliwekwa mnamo 2020-02-11.