Mali (kipindi cha runinga)
Mali ni kipindi cha runinga kinachorushwa na stesheni ya NTV (Kenya). Wito wake kwa Kiingereza ni "United by Blood: Divided by Greed" (Kuunganishwa kwa damu; kutenganishwa kwa tamaa). Mali ilianza kurushwa nchini Kenya halafu nchini Uganda. Kipindi kilirushwa miaka 2011-2015.[1] Ki kipindi cha aina yake, huoneshwa mara tatu kwa wiki [2]
Hadithi
hariri"Mali" inafuatilia maisha ya jamaa tajiri kabisa lakini inayosumbuliwa na mambo ya ndani. Mzee wa nyumba meoa wanawake zaidi ya mmoja na anaendesha nyumba yake kama kambi ya kijeshi.
Ndugu hao wanatofautiana kitabia, kitamaduni, kijamii na hali ya kimaisha lakini wote wanazo hadithi motomoto kuhusu mapenzi, pesa, nguvu, kutongozana na mafanikio.
Hadithi inachacha pale ambapo mzee wa nyumba, Bw. G Mali, anaanguka na kuaga dunia kabla ya kuwacha wasia. Anawacha jamaa mbili katika tamaa, ubatilifu, kugawanyika na pia kugunduliwa kwa siri nzitonzito za kijamaa na za kibinafsi.
Mali ni hadithi ya tamaa ya kufanya kinachofaa na mambo yote yanayohusu mwendo huo. MALI inapeleka mtazamaji katika mwendo wa kuonyesha dubwana za jamii hiyo, jamaa na umbali mtu anaweza kuenda katika kutafuta mapenzi, pesa na furaha iliyoje.
Mali inaonyesha upande mwingine wa utajiri pasi na ukweli wa jamaa waliotengana na njia tofauti kila ndugu anafanya ili kuiunganisha ilhali kuna tofauti nyingi.
Wahusika
haririWahusika Wakuu
haririG Mali -George Ohawa
Mabel Mali -Mary Gacheri
Usha Mali -Mkamzee Mwatela
Bella -Carolyne Midimo
Nandi Mali -Mumbi Maina
Lulu Mali -Brenda Wairimu
Richard Mali -Kevin Samuel
Arthur Mali -Daniel Peter
Wahusika wadogo
haririMwambu -Abel Amunga
Tony -Tonie Mwangi
Lucia -Kate Khasoa-Kole
Fadhili -Conrad Makeni
Don -Gerald Langiri
Bishop -David Gitika
Clara -Natasha Likimani
Zolo -Hamza Omar
Ron -Nic Wang’ondu
Nikita -Marilyn Perez
Miriam -Joan Arigi
Selena -Carolyne Ngorobi
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Feature article on Nation Media Ilihifadhiwa 28 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine.
- Variety International
- Kenyan Actors
Makala hii kuhusu kipindi fulani cha televisheni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mali (kipindi cha runinga) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |