Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.[1]
TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mamlaka na malengo
haririMamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
- Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
- Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
- Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
- Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
- Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
- Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
- Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
- Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.
Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
- Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
- Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
- Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
Tanbihi
hariri- ↑ "Tanzania Communications Regulatory Authority". Commonwealth of Nations (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-06-30.