Mankato Free Press

The Free Press ni gazeti linalochapishwa kila siku katika eneo la Mankato , Minnesota.

Mankato Free Press
Jina la gazeti Mankato Free Press
Aina ya gazeti Gazeti la kuchapisha kila siku
Lilianzishwa 4 Aprili 1887
Eneo la kuchapishwa Mankato hasa Miji mikubwa ya Mankato, Mankato Kaskazini
Waseca, St Peter na Le Suerer
Nchi Marekani Marekani
Mwanzilishi L.P. Hunt
Mhariri Joe Spear
Mmiliki Kampuni ya Magazeti ya Community (CNC)
Mchapishaji Jim Santori
Makao Makuu ya kampuni Mankato, Minnesota
Nakala zinazosambazwa 22,000
Lilikwisha *.Mankato magazine(usambazaji wa nakala 10,000)
*.The Land (usambazaji wa nakala 35,000).
Tovuti http://www.mankatofreepress.com

Kuhusu Gazeti Hili

hariri

Mnamo 4 Aprili 1887, Mhariri L.P. Hunt alichapisha toleo la kwanza la Mankato Daily Press na akagundua halikuwa kazi rahisi. Katika kuomba msamaha kutoka kwa wasomaji wake, Hunt aliandika, "Kazi ya kuchapisha idadi ya hapo awali ya nakala za gazeti hili ni gumu kuliko watu wasiohusika na kazi ya magazeti wanavyojua ama wanavyoambiwa kuwa. Ukweli ni kuwa gazeti la leo la Daily Free Press limekuwa fupi kwa matumizi ya telegrafia ,na vilevile vitu vingine lakini bado lilikuwa ngumu kwa wafanyikazi wetu kulichapisha na tunaomba kuwa watu watatuvumilia siku moja au mbili tukiwa tukinyoosha 'mercheen' zetu." Tangu wakati ule, 'mercheen' imeendelea kuchapisha magazeti yao katika eneo la Mankato kwa miaka 100 bila shida yoyote.

Chapisho la seminali lilikuwa Independent lililoanza kuchapishwa katika mwaka wa 1857. Miaka sita baadaye, jarida hili lilinunuliwa na Charles Slocum na likaitwa Mankato Union. Kisha katika mwaka wa 1880, gazeti la Union na gazeti shindani lake katika eneo la Mankato, Record yakaungana na kuwa gazeti la wiki la Mankato Weekly Free Press. Liliendelea kama gazeti la wiki hadi mwaka wa 1887 lilipokuwa gazeti la kila siku. Lilianza kama gazeti la kihafidhina la Republican na likabaki kuwa hivyo hadi sasa. Katika mwaka wa 1970, gazeti lilitoa neno "Mankato" kutoka jina lake. Neno "Daily" lilikuwa limeondolewa katika mwaka wa 1940.

Mmiliki wa mwisho wa gazeti hili alikuwa Jared How, aliyeuza kampuni ya The Free Press kwa Shirika la Ottaway Newspapers (kitengo cha kampuni ya Dow Jones na Wenzake). Ottaway ilinunua asilimia 11 ya kampuni hiyo katika mwaka wa 1977 na asilimia ilyobaki katika mwaka wa 1979. Katika mwaka wa 2002, Ottaway iliuza The Free Press na magazeti mengine kwa Shirika la Community Newspaper Holdings. Katika mwaka wa hamsini wa uchapishaji wa gazeti hili, usambazaji wa The Free Press ulikuwa nakala 12,000; hivi leo usambazaji wake ni nakala 22,629 kila siku. Huchapisha ,pia, magazeti ya Mankato Magazine na The Land- gazeti kuhusu ardhi na vijiji katika eneo la Minnesota. Hutumikia wasomaji wake kwa tovuti ya http://www.mankatofreepress.com iliyoanzishwa katika mwaka wa 1994 na hivi sasa hii ndiyo tovuti maarufu katika eneo hilo.

Katika Gazeti

hariri

Wafanyikazi wa The Free Press huhudumia makata 6 - Blue Earth, Nicollet, Le Sueur, Brown, Waseca na Watonwan. Miji mikubwa ya Mankato, Mankato Kaskazini, Waseca, St Peter na Le Suerer ,pia, huwa maeneo ya usambazaji. Gazeti hilo linajisifu kwa makala na picha zilizotuzwa tuzo mbalimbali. Gazeti hili huchapisha habari za michezo na habari za Chuo Kikuu cha Minnesota na habari za Mankato. Gazeti hili huchapisha Mankato magazine(usambazaji wa nakala 10,000) na The Land (usambazaji wa nakala 35,000).

Viungo vya nje

hariri