Mapouka (pia inajulikana kwa jina la Macouka) ni ngoma ya dansi ya kimila ambayo inatokea katika eneo la Dabou huko mjini kusini-mashariki mwa nchi ya Côte d'Ivoire. Wakati mwingine ngoma hii huchezwa pia wakati wa sherehe za kidini. Pia inajulikana kwa jina la "La danse du fessier" au "dansi ya kinyumenyume".

Dansi hii huwa na koreografia yenye mtawasha wa kimahaba hakuna tena mfano. Dansi hii hasa uhusisha wanawake wakitingisha matako yao, nginjanginja, huku wakiyalekeza upande wa watazamaji wao. Katika miaka ya 1980, wasanii wengi wa Ivory Coast walijaribu kuupatia umaarufu mtindo huu, lakini hawakufanikiwa kabisa. Miongoni mwa makundi yaliyowahi kupata umaarufu ni pamoja na Tueuses de Mapouka.

Kuna aina mbili ya dansi hii, ile ya awali na ya hii ya kisasa. Dansi ya kisasa huchezwa na vijana wadogo ambao wengi wametia chumvi kupindukia hadi kuonekana kama sivyo inavyotakiwa ichezwe kulingana na pendekezo la chimbuko la ngoma hii.

Mwaka wa 1998, serikali ya Côte d'Ivoire imeamua kukataza kabisa utumbuizaji wake katika umma. Ni mwiko kufanya mbele ya hadhara, na kwa kufuatia ukatazaji huu umepelekea dansi hii kukua kwa kasi kimataifa, hasa katika nchi za Jangwa la Sahara na mataifa mengine ya magharibi yenye idadi kuwa ya wasemaji wa Kifaransa.

Marejeo

hariri