Marjarini
(Elekezwa kutoka Margarine)
Marjarini (kutoka Kiingereza "Margarine") ni mafuta ya kuliwa yaliyobuniwa kama mbadala wa siagi. Iko katika hali laini kiasi, ili iweze kupakuliwa kwa jotoridi la wastani. [1] Hutengenezwa kwa kutumia uto (mafuta ya mimea) au pia kwa kutumia mafuta ya nyama. Inaweza pia kuwa na unga wa maziwa, chumvi na dawa ya emulshani. Marjarini hutumiwa katika vyakula vingi vilivyookwa kiwandani.
Marjarini ilibuniwa pale Ufaransa katika miaka ya 1860, wakati serikali ilitafuta mafuta mbadala kwa ajili ya jeshi yasiyoharibika haraka.[2] [3].
Katika Afrika ya Mashariki marjarini hujulikana mara nyingi kwa jina la blubendi (blue band) kutokana na rajamu ya marjarini inayouzwa sana.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marjarini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |