Marianne Bachmeier
Marianne Bachmeier (3 Juni 1950 – 17 Septemba 1996) alikuwa mwanamke kutoka Ujerumani Magharibi aliyempiga risasi na kumuua Klaus Grabowski, mwanamume aliyeshtakiwa kwa kubaka na kuua binti yake Anna (14 Novemba 1972 – 5 Mei 1980).
Tukio hilo lilihesabiwa kama kitendo cha kujichukulia sheria mkononi mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Lübeck mwaka 1981. Kesi hiyo ilizua mjadala mzito katika umma. Vyombo vya habari vilijikita katika kuripoti kila hatua.
Hata hivyo, matokeo ya hukumu yalisomeka ya kwamba kilikuwa kitendo cha kuua bila kukusudia na kumiliki silaha kinyume cha sheria. Alifungwa miaka sita na kuachiliwa kwa masharti baada ya kutumikia miaka mitatu. Bachmeier alihamia nje ya nchi lakini alirudi Ujerumani baada ya kugunduliwa kuwa na saratani ya kongosho. Alifariki akiwa na umri wa miaka 46 na alizikwa kando ya kaburi la binti yake wa miaka saba, Anna, katika Makaburi ya Burgtor, Lübeck.
Maisha ya awali na familia
haririMarianne Bachmeier alizaliwa tarehe 3 Juni 1950.[1][2] Alikulia mjini Sarstedt, mji mdogo karibu na Hildesheim, Lower Saxony, Ujerumani ya Magharibi, ambako wazazi wake walikimbilia kutoka Prussia ya Mashariki baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Bachmeier alikulia katika nyumba ya kihafidhina na wazazi wenye msimamo mkali wa kidini.[3] Baba yake, ambaye awali alikuwa mwanachama wa Waffen-SS,[3] alikuwa mbaguzi, mlevi ambaye alitumia muda mwingi kwenye baa karibu na nyumba ya familia.[4] Mazingira ya nyumbani yalikuwa mabaya, na ulevi ulimfanya baba yake kuwa na hasira zaidi.[4] Wazazi wake walitalikiana, na mama yake aliolewa tena baadaye.[3][4] Bachmeier alikulia katika malezi ya shida. Alikuwa na baba wa kufikia katili na mwishowe ndoa mpya ya mamake ikaelekea jongomeo. Walitimuliwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi.[3][4]
Mnamo mwaka 1966, akiwa na umri wa miaka 16, Bachmeier alipata mtoto wake wa kwanza wa kuasili tangu akiwa mchanga.[3] Alipata ujauzito tena akiwa na umri wa miaka 18 na mpenzi wake.[3] Bachmeier alibakwa muda mfupi kabla ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa pili.[5] Mtoto wake wa pili pia alitolewa kwa kuasili alipokuwa mchanga.[5]
Bachmeier alichumbiwa na meneja wa Tipasa, baa ambayo walikuwa wakifanya kazi wote mnamo mwaka 1972.[5][6] Alipata ujauzito kwa mara ya tatu akiwa na umri wa miaka 22.[5][6] Tarehe 14 Novemba 1972, mtoto wa tatu wa Bachmeier, Anna, alizaliwa, na alimlea akiwa mwenyewe.[5][6] Kwa hivyo, Bachmeier alikuwa akienda na Anna kazini. Pia ilisemekana kuwa hakukuwa na haja ya kurudi nyumbani haraka baada ya muda wake wa kazi kuisha.[7]
Mauaji ya binti yake
haririMnamo Mei 5, 1980, wakati Anna alipokuwa na umri wa miaka saba, aligombana na mama yake na kuamua kutoroka shule.[8][9] Siku hiyo, alitekwa nyara na Klaus Grabowski, mchinjaji mwenye umri wa miaka 35, ambaye nyumba yake alikuwa ameitembelea hapo awali kucheza na paka wake.[8][9] Alimshikilia Anna kwa saa kadhaa nyumbani kwake, akamnyanyasa kingono na hatimaye kumkaba kwa kutumia soksi za mchumba wake.[10][11] Kulingana na mwendesha mashtaka, Grabowski alimfunga Anna na kuweka mwili wake ndani ya sanduku, kisha akaliacha kando ya mfereji. Mchumba wa Grabowski alimripoti kwa polisi.[10][11]
Grabowski alikuwa mhalifu wa ngono aliyewahi kuhukumiwa kwa unyanyasaji wa wasichana wawili.[12] Mnamo 1976, alikubali kuhasiwa kwa kutumia kemikali, ingawa baadaye alifanyiwa matibabu ya homoni kurejesha uwezo wake wa kihisia.[12][13] Baada ya kukamatwa, Grabowski alidai kwamba Anna alikuwa amejaribu kumshawishi kwa kumtishia kwamba angemwambia mama yake kuhusu unyanyasaji huo.[14] Alisema kwamba alimuua kwa sababu aliogopa kurudi gerezani.[14]
Kujichukulia sheria mkononi mahakamani
haririMnamo saa 4 asubuhi tarehe 6 Machi 1981, siku ya tatu ya kesi hiyo,[15] Bachmeier alifanikiwa kuingia na bastola ya aina ya Beretta 70[16] katika chumba cha mahakama ya Wilaya ya Lübeck, chumba namba 157, na kumpiga risasi Grabowski hadi kufa.[17][18]
Alielekeza bastola kwenye mgongo wake na kufyatua risasi saba; sita zilimpiga Grabowski, alikufa papo hapo.[19][20] Baada ya tukio hilo, Bachmeier alishusha bastola yake na alikamatwa bila upinzani.[15][19]
- Katika filamu mbili za hali halisi za mwaka 1984, No Time for Tears: The Bachmeier Case na Anna's Mother, Bachmeier alionyeshwa kama mama asiye na mume aliyefanya kazi hadi usiku wa manane na kisha kulala mchana, akiwaacha binti yake wa miaka saba peke yake wakati wa mchana.[21][6] Bachmeier alikuwa akifahamu mtindo wake wa maisha wenye matatizo na alitaka kumtoa Anna kwa kuasili.[21] Marafiki walidai kuwa alimchukulia Anna kama mtu mzima mdogo, na tangu umri mdogo.
Marejeo
hariri- ↑ Langenscheid, Adrian; Rickert, Benjamin; Löschmann, Stefanie (2022-06-18). True Crime Deutschland 3 Wahre Verbrechen – Echte Kriminalfälle: Ein erschütterndes Portrait menschlicher Abgründe (kwa Kijerumani). BoD – Books on Demand. ISBN 978-3-7546-5920-5.
- ↑ Nordiske Kriminalsaker 1985 (kwa Kinorwe). Lindhardt og Ringhof. 2017-01-02. ISBN 978-87-26-09361-2.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 Haas, Nicole E.; de Keijser, Jan W.; Bruinsma, Gerben J. N. (2012-12-01). "Public support for vigilantism: an experimental study". Journal of Experimental Criminology (kwa Kiingereza). 8 (4): 387–413. doi:10.1007/s11292-012-9144-1. ISSN 1572-8315. S2CID 255134224. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Machi 2023. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2023.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 "Countdown mit Annas Mutter", Der Spiegel, 1984. (de)
- ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Karomo, Chege (2023-01-19). "Did Marianne Bachmeier go to jail? Her crime detailed". OkayBliss (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 2023-01-28.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 6.2 6.3 Driest, Burkhard, mhr. (1984), Annas Mutter [Anna's Mother] (kwa Kijerumani), MUBI, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Oktoba 2022, iliwekwa mnamo 2023-02-02
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Der Fall Marianne Bachmeier: Selbstjustiz einer Mutter" [The case of Marianne Bachmeier: Vigilante justice of a mother]. Norddeutscher Rundfunk (kwa Kijerumani). 2023-01-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Februari 2023. Iliwekwa mnamo 2023-02-01.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 8.0 8.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named:10
- ↑ 9.0 9.1 "Kalenderblatt: 2.3.1983 Justiz und Selbstjustiz", Der Spiegel, 2008-03-02. (de)
- ↑ 10.0 10.1 Bilderbeck, Poppy (2022-12-31). "Mother who got her revenge by firing seven shots in front of packed courtroom". UNILAD (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 2023-01-24.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 11.0 11.1 ""Ich schäme mich, ich schäme mich so": Gerhard Mauz zum Fortgang des Strafverfahrens gegen Marianne Bachmeier in Lübeck", Der Spiegel, 1982-01-03. (de)
- ↑ 12.0 12.1 ""Ohne kollegiale Rücksichtnahme": Spiegel-Reporter Gerhard Mauz im Prozeß gegen Marianne Bachmeier in Lübeck" ["Bila kujali wenzake": Ripota wa SPIEGEL Gerhard Mauz katika kesi ya Marianne Bachmeier huko Lübeck], Der Spiegel, 1982-11-07, ISSN 2195-1349, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Desemba 2022, iliwekwa mnamo 2021-12-02
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Marianne Bachmeier; "Revenge Mother" Who Shot her Daughter's killer" (kwa American English). 2023-04-29. Iliwekwa mnamo 2023-05-08.
- ↑ 14.0 14.1 Ishak, Natasha (2021-02-02). "Meet The German 'Revenge Mother' Who Shot Her Daughter's Killer in the Middle of His Trial". All That's Interesting (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2023. Iliwekwa mnamo 2023-01-21.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 15.0 15.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named:72
- ↑ "Museen Nord: Pistole" [Museen Nord: Bastola]. UNSEEN NORD (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Novemba 2022. Iliwekwa mnamo 2022-11-17.
- ↑ Hilger, Maternus (2021-06-03). "Berühmter Kriminalfall: Marianne Bachmeier tötet Mann im Gericht" [Kesi maarufu ya uhalifu: Marianne Bachmeier amuua mwanaume mahakamani]. Express (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Februari 2022. Iliwekwa mnamo 2022-02-03.
- ↑ "Die spektakulärsten Kriminalfälle: Dem Verbrechen auf der Spur, Teil 2", Der Spiegel, 2015-07-22. (de)
- ↑ 19.0 19.1 Evans, Stephen. "The Nazi murder law that still exists", Berlin: BBC News, 5 Februari 2014.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs named:13
- ↑ 21.0 21.1 Bohm, Hark (1984). "Der Fall Bachmeier – Keine Zeit für Tränen | filmportal.de" [The Bachmeier case – no time for tears]. Filmportal. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Februari 2023. Iliwekwa mnamo 2023-02-02.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)