Marielle Francisco da Silva (27 Julai 1979 - 14 Machi 2018) alikuwa mwanasiasa, mwanaisimu, mfeministi, msoshalisti na mtetezi wa haki za binadamu kutoka Brazil. Franco alihudumu kama mshauri wa jiji katika Baraza la Manispaa la Rio de Janeiro kwa chama cha Socialism and Liberty Party (PSOL) kuanzia Januari 2017 hadi kuuawa kwake.

Tarehe 14 Machi 2018, wakati akiwa kwenye gari baada ya kutoa hotuba kaskazini mwa Rio de Janeiro, Franco na dereva wake walipigwa risasi mara kadhaa na kuuawa na wauaji wawili waliokuwa wakisafiri kwenye gari jingine. Franco alikuwa mkosoaji mwenye sauti juu ya ukatili wa polisi na mauaji yasiyo ya kisheria, pamoja na uingiliaji kati wa shirikisho la mwezi Februari mwaka 2018 uliofanywa na rais wa Brazil Michel Temer katika jimbo la Rio de Janeiro ambao ulisababisha kupelekwa kwa jeshi katika operesheni za polisi. Mnamo Machi 2019, maafisa wawili wa zamani wa polisi walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya Marielle Franco.