Mario Das Neves (amezaliwa 27 Aprili 1951) ni mwanasiasa wa Argentina mwanachama wa Chama cha Justicialista. Yeye ni Gavana wa jimbo la Chubut katika nchi ya Argentina.

Mario Das Neves
Gavana wa Chubut
Muda aliokuwa ofisini
2003-
Tarehe ya kuingia ofisi: 10 Desemba 2003
Kabla yake: José Luis Lizurume
Kibinafsi
Alizaliwa: 27 Aprili 1951 (1951-04-27) (umri wa miaka 58)
Eneo la kuzaliwa: Avellaneda,Buenos Aires
Msimamo wake wa siasa: Kiperonisti
Uzalendo: Argentina

Das Neves alizaliwa Avellaneda, katika eneo la Gran Buenos Aires, na kukulia katika Santa Fe lakini alihamia Chubut akiwa na umri wa miaka 20 ili kujaribu kuwa mwanakandanda wa Huracán de Trelew bila mafankio. Alihusika sana katika kikundi cha vijana wa Kiperonisti na ilipofika mwaka wa 1987 alikuwa amepata jukumu muhimu katika utawala wa Trelew akiwa chini ya Nestor Perl.

Wasifu

hariri
 
Mario Das Neves

Katika mwaka wa 1991, Das Neves alikuwa mgombea wa kiti cha meya wa Trelew na kashinda duru ya kwanza lakini akashindwa katika duru ya pili. Mwaka uliofuata, akawa kiongozi wa Chama cha Justicialista katika tawi la Chubut. Alichaguliwa kuwa katika Chemba ya Argentina ya Manaibu akiwakilisha Chubut katika mwaka wa 1995. Alipochaguliwa alianza kampeni kali dhidi ya ufisadi katika operesheni ya forodha katika Buenos Aires na akaongoza tume ya uchunguzi iliyosababisha kushtakiwa kwa watu kadhaa. Yeye alitajwa kuwa naibu bora kabisa katika mwaka wa 1997. Katika mwaka wa 1999, alichaguliwa tena kama naibu na akawa mwenyekiti wa kwanza wa kamati ya kulinda wateja.

Katika mwaka wa 2001, katika urais mfupi wa Adolfo Rodríguez Saá,Das Neves aliteuliwa kama Waziri wa Forodha na hivyo basi akajiuzulu kutoka Congress. Siku chache baadaye baada ya Eduardo Duhalde kuwa rais, aliendelea kuwa na Das Neves kama Waziri wa Forodha. Hata hivyo,alipingana na Roberto Lavagna na akaanza kutafuta pahali pengine pa kuendeleza kazi yake.

Das Neves aligombea kiti cha gavana wa Chubut katika mwezi wa Novemba 2003 dhidi ya gavana wa wakati huo wa UCR, José Luis Lizurume. Das Neves aliuungwa mkono na Mperonisti mwenzake,Rais mpya Néstor Kirchner. Shindano lake na Lizurume lilikuwa la karibu,Das Neves akishinda kwa 45.6% dhidi ya 41.3%.

Das Neves amemaliza 80% ya kusomea digrii ya somo la sheria. Amemwoa Raquel Di Perna na wana watoto wawili.

Viungo vya nje

hariri