Martin Benjamin
Dakta Martin Benjamin ni mwanzilishi wa mradi wa kamusi huru, The Kamusi Project (Mradi wa Kamusi Hai ya Kiswahili Kwenye Mtandao). Martin kitaaluma ni mwana anthropolojia ambaye amefanya utafiti kwa miaka mingi nchini Tanzania.
Wazo la kuwa na kamusi mpya ya Kiswahili lilimjia mwaka 1993. Akishirikiana na Ann Biersteker walianzisha The Kamusi Project mwanzoni mwa mwaka 1995. Hivi sasa yeye ni mhariri wa mradi huo ambao uko katika Chuo Kikuu cha Yale, nchini Marekani.
Mwaka 2004 akishirikiana na Alberto Escudero-Pascual walitengeneza programu ya Tuksi Koti la Rangi kama zawadi kwa ajili ya mradi wa Kamusi Hai Ya Kiswahili Kwenye Mtandao.
Viungo vya nje
hariri- Kamusi Hai ya Kiswahili Kwenye Mtandao Ilihifadhiwa 15 Novemba 2007 kwenye Wayback Machine.