Maseru ni mji mkuu wa Lesotho ikiwa na wakazi 174.000 Einwohner (2003). Chuo Kikuu cha Lesotho na kiwanja cha kimataifa cha ndege ni karibu na mji. Maseru iko kwa mto Caledon (Mohokare). Ni mji mkubwa wa pekee nchini.

Jiji la Maseru
Nchi Lesotho
Barabara kuu ya kuelekea kusini ya Maseru
Maseru katika Lesotho

Historia

hariri

Ilikuwa kituo kidogo cha biashara ilipoteuliwa na chifu Moshoeshoe I. wa Wasotho kuwa mji mkuu wake mwaka 1869.

Tangu 1884 hadi 1966 ilikuwa mji mkuu wa nchi ya kulindwa chini ya Uingereza ya "Basutoland". 1966 ikawa mji mkuu wa Lesotho huru.

Uchumi

hariri

Kuna viwanda vya kutengenezea mishumaa na matandiko ya zulia. Kuna pia viwanda vya vitambaa kwa ajili ya soko la Marekani.