Mataifa Yanayostawi ya G20

G20 (Kikundi cha memba 20, pia G21, G22 na G20 +) ni kambi ya mataifa yanayostawi iliyoanzishwa tarehe 20 Agosti 2003.

     Mataifa yanayostawi yaliyo memba wa kudumu wa G20      Mataifa yanayostawi yasiyo memba wa kudumu wa G20

Kundi hili liliibuka katika mkutano wa tano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), uliofanyika mjini Cancun, Mexico kuanzia 10 Septemba hadi 14 Septemba mwaka 2003.

G-20 ina asilimia 60 ya watu wote duniani, asilimia 70 ya wakulima na asilimia 26 ya mauzo ya kilimo duniani [1]

Historia

hariri

Chanzo chake kilikuwa mwezi Juni 2003, ambapo mawaziri wa kigeni kutoka Brazili, India na Afrika ya Kusini walitia saini tamko lijulikanalo kama Tamko la Brasilia [2] ambapo walidai kuwa

"washirika wakuu wa biashara bado wanaadhiriwa na shaka ya kulinda kwenye sekta zenye ushindani mdogo za mataifa yao [...] na kutilia mkazo umuhimu wa matokeo ya duru ya sasa ya mazungumzo ya biashara hasa kwa kutoa sera ya kulinda na mazoea ya kuharibu biashara [...] Aidha mataifa ya Brazili, India na Afrika Kusini yaliamua kuweka pamoja mipango yao ya biashara huru."

Kwa sasa, Kikundi hiki kinajumuisha mataifa 23 :

  1.   Argentina
  2.   Bolivia
  3.   Brazil
  4.   Chile
  5.   China
  6.   Kuba
  7.   Ekuador
  8.   Misri
  9.   Guatemala
  10.   Uhindi
  11.   Indonesia
  12.   Mexiko
  13.   Nigeria
  14.   Pakistan
  15.   Paraguay
  16.   Peru
  17.   Philippines
  18.   Afrika Kusini
  19.   Tanzania
  20.   Uthai
  21.   Uruguay
  22.   Venezuela
  23.   Zimbabwe

Hata hivyo, muonekano "rasmi" wa G-20 ulitokea kama jibu kwa nakala iliyotolewa tarehe 13 Agosti 2003 na Jumuiya ya Ulaya (EC) na Marekani iliyokuwa na pendekezo sawa la kilimo kwa mkutano wa mawaziri mjini Cancun.

Mnamo tarehe 20 Agosti 2003, hati iliyotiwa saini na nchi ishirini na kutolewa tena kama hati ya mkutano wa mawaziri wa Cancun mnamo tarehe 4 Septemba ilipendekeza mbadala kiunzi kwa ule wa EC na Marekani kuhusu kilimo kwa mkutano wa Cancun.

Hati hii iliashiria mwanzo wa G-20. Wasajiliwa wa awali wa kundi, kwenye hati ya 20 Agosti 2003, walipitia mabadiliko mengi, huku wakijulikana kwa majina tofauti kama vile G-21 au G-22. Jina G-20 mwishowe lilichaguliwa, kwa heshima ya tarehe kikundi kilipoanzishwa.

Tangu lianzishwe, kundi hili limekuwa na uanachama usio thabiti. Wanachama wa awali walikuwa ni pamoja na: Colombia, Costa Rica, Ecuador, El Salvador, Peru, na Uturuki.

Kufikia Oktoba 2008, kundi hili lilikuwa na wanachama 23.

Msingi wa uongozi wa G-20, unaojulikana kama kambi ya G4, unajumuisha Brazili, China, India na Afrika ya Kusini.

Tanbihi

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-08-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-19.
  2. IBSA - utatu, mpango wa maendeleo kati ya India, Brazil na Afrika ya Kusini

Viungo vya nje

hariri