Mathare United
Mathare United ni klabu ya kandanda nchini Kenya yenye makazi katika mtaa wa mabanda wa Mathare katika mji mkuu wa Nairobi. Wao ni mwanachama wa zamu wa ligi kuu ya Kenya katika kandanda la Kenya. Uwanja ambao wao hutumia kwa mechi zao za nyumbani ni Moi International Sports Centre. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1994 kama klabu ya utaalamu kwa Mathare Youth Sports Association (MYSA) (ambayo ilianzishwa mwaka 1987).
|
Mwaka 1996 klabu hii ilishinda ligi ya mkoa wa Nairobi na kupandishwa hadi ligi ya National Super League Kigezo:Uthibitisho unahitajika. Mathare United ilishinda Kombe la Kenya mwaka wa 1998, wakati bado walikuwa wanasakata kabumbu katika divisheni ya pili. Klabu hii imekuwa katika Ligi kuu ya Kenya tangu mwaka wa 1999. Klabu hii ilishinda tena Kombe la Kenya kwa mara ya pili mwaka wa 2000 Kigezo:Uthibitisho unahitajika
Mpango unaoendelea wa vijana wa MYSA imewatengeneza wachezaji wengi wa Kenya, kwa mfano Dennis Oliech. Mwennyekiti wa Mathare United ni Bob Munro.
Timu ya vijana ya Mathare United, Mathare Youth ilipandishwa ngazi katika ligi kuu ya Kenya mwaka wa 2005. Mathare Youth inaendeshwa kama klabu ya kandanda tofauti.
Majalio
hariri- Ligi kuu ya Kenya:1
-
- 2008
- Kombe la Rais:2
-
- 1998, 2000
Utendaji katika mashindano ya CAF.
hariri- Ligi ya mabingwa ya CAF : Wameshiriki mara 1
-
- 2008 - Raundi ya mchujo
- Kombe la CAF : Wameshiriki mara 1
-
- 2002 - Raundi ya kwanza
- Kombe la CAF la Washindi:Wameshiriki mara 2
-
- 1986 - Raundi ya Pili
- 1971: Raundi ya kwanza
- 1986 - Raundi ya Pili
Marejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu timu ya mpira wa miguu ya Kenya bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |