Matola ni kata ndani ya Mji wa Njombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania yenye postikodi namba 59118 .

Kata ya Matola
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Njombe
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 12,262

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,262 [1] walioishi humo.

Kata hiyo inaundwa na vijiji vya Matola, Mtila, Boimanda, Kitulila na Mbega.

Kijiji cha Kitulila ni kijiji muhimu zaidi kwa kata ya Matola kwa kuwa ndicho cha pili kwa ukubwa na kipo katikati ya barabara kuu ya Njombe kuelekea Ludewa hadi mwambao mwa ziwa Nyasa (Manda).

Wakazi wake wengi ni Wabena (kwa asilimia zaidi ya 90), halafu Wakinga na Wapangwa.

Shughuli kubwa za wakazi wa kijiji hicho ni kilimo cha viazi mviringo, mahindi, matunda aina ya tufaa, upandaji wa miti aina ya Pines. Upande wa mashamba kuna shamba kubwa la Chai Estate ya Dansland ambalo ni tawi la Luponde Tea Estate. Kwa hakika kijiji hiki kimejaliwa ardhi nzuri yenye rutuba na wakazi wake wengi ni watu wenye bidii.

Pia ndani ya kijiji hicho kuna shirika la Watawa wa Mtakatifu Agnes nyumba ya Mtakatifu Getrude Imiliwaha. Pia kuna sekondari Moja ya wasichana ya Mtakatifu Getrude inayomilikiwa na Watawa hao. Pia kuna shule za msingi mbili: Shule ya msingi Kona na Shule ya Msingi Kitulila.

Upande wa imani wakazi wake kwa asilimia 98 ni Wakristo wa madhehebu ya Kikatoliki, Waanglikana na Walutheri kwa idadi ndogo. Kuna makanisa rasmi matano: Kanisa Katoliki likiwa na makanisa manne na Anglikana moja, lakini pia kuna makanisa madogo yasiyo na usajili, mengi yakiwa ni madhehebu ya Kipentekoste, lakini mwitikio wake ni mdogo kiasi cha makanisa hayo kuibuka na kupotea.

Marejeo hariri

  1. Sensa ya 2012, Njombe - Njombe TC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-29.
  Kata za Wilaya ya Njombe Mjini - Tanzania  

Ihanga | Iwungilo | Kifanya | Lugenge | Luponde | Makowo | Matola | Mji Mwema | Njombe Mjini | Ramadhani | Utalingolo | Uwemba | Yakobi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Matola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.