Mauaji ya Jordan Davis

Mauaji ya mtoto wa kimarekani mwaka 2012

Mnamo 23 novemba,2012, Jordan davis mwanafunzi mweusi wa daraja la pili mwenye umri wa miaka 17, aliuwawa katika kituo cha mafuta cha Gate Petroleum katika mji wa Jacksonville, Florida na Michael David Dunn, mtengenezaji wa programu mweupe mwenye umri wa miaka 45,kufuatia mabishano juu ya muziki wa sauti uliopigwa na Davis na marafiki zake watatu. Dunn alipatikana na hatia kwa makosa matatu ya jaribio la mauaji ya mwanafunzi wa daraja la pili.

Baraza la majaji halikuweza kufikia uamuzi wa kumhukumu Dunn kwa mauaji ya Davis katika kesi ya kwanza. Katika kesi ya pili, Dunn alipatikana na hatia ya mauaji ya daraja la kwanza ya Davis na kuhukumiwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa msamaha pamoja na kifungo cha miaka 105 gerezani, ambayo ni vifungo viwili vya maisha mfululizo.[1][2]

Historia hariri

Dunn na mchumba wake Rhonda Rouer walisafiri kutoka nyumbani kwao ili kuhudhuria harusi ya mwana wa zamani katika Orange Park, karibu na Jacksonville, Florida. Dunn na Rouer waliondoka kwenye harusi mapema ili kurudi kwenye hoteli yao na kumtunza mtoto wao wa miezi sita. Walipokuwa wakirudi hotelini mwao, wawili hao waliamua kusimama katika kituo cha mafuta cha Gate Petroleum ili kupata chupa ya divai.[3] Tommie Stornes, Leland Brunson, Jordan Davis, na Tevin Thompson walikuwa wametumia siku nzima kusafiri katika maduka mbalimbali ndipo walipoamua kwenda kwenye kituo cha mafuta cha Gate Petroleum ili kununua sigara.[4]

Marejeo hariri

  1. A. B. C. News. "'I Was the Victim,' Says Loud Music Trial Shooter in Jailhouse Phone Call". ABC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-16. 
  2. https://efactssc-public.flcourts.org/casedocuments/2019/2063/2019-2063_notice_88213_notice2ddiscretionary20juris2028direct20conflict29.pdf
  3. The Case of Michael Dunn (kwa sw-TZ), iliwekwa mnamo 2022-04-16 
  4. Eliott C. McLaughlin (2014-02-06). "Did Jordan Davis have weapon? Attorneys spar in loud music murder trial". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-16.