Mavakamteni
Mavakamteni (kwa Kiingereza: Mavacamten) inayouzwa kwa jina la chapa Camzyos, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa moyo na mishipa.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kizunguzungu na kupoteza fahamu kwa muda kwa sababu ya kushuka kwa shinikizo la damu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kushindwa kwa moyo.[1] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[1] Dawa hii ni kizuizi cha mayosini (myosin) ya moyo.[1]
Mavakamteni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2022.[1] Imekuwa haipatikani Ulaya au Uingereza kufikia mwaka wa 2022.[2] Nchini Marekani, mwezi mmoja wa dawa hii hugharimu takriban dola 7,800 za Kimarekani. [3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Camzyos- mavacamten capsule, gelatin coated". DailyMed. 28 Aprili 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Mavacamten". SPS - Specialist Pharmacy Service. 19 Oktoba 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Juni 2022. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Camzyos Prices, Coupons, Copay & Patient Assistance". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Mei 2023. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)