Nchi za Maziwa Makuu
(Elekezwa kutoka Maziwa makubwa ya Afrika)
Nchi za Maziwa Makuu ni nchi zinazopakana na maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na Uganda.
Kati ya maziwa makubwa yaliyoko katika eneo hili kuna
- Ziwa Nyanza (Viktoria)
- Ziwa Tanganyika
- Ziwa Nyasa (Malawi)
- Ziwa Mwitanzige (Albert)
- Ziwa Rutanzige (Edward)
- Ziwa Kivu
- Ziwa Turkana
Eneo hili ni muhimu kimataifa kutokana na bioanwai kubwa: asilimia 10 ya spishi za samaki wote duniani zinapatikana katika maziwa yake.
Maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa hushika robo moja ya maji matamu (yasiyo maji ya chumvi) yaliyopo duniani kote.
Marejeo
hariri- Jean-Pierre Chrétien. The Great Lakes of Africa: Two Thousand Years of History trans Scott Straus
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nchi za Maziwa Makuu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |