Mazoezi ya mwili
Mazoezi ya mwili (kwa Kiingereza "physical exercises") ni vitendo vinavyofanywa aghalabu na watu au mtu ili kuuweka mwili katika hali ya afya nzuri na kuwa tayari kwa ajili ya jambo maalumu.


Inafaa uanze mazoezi hayo kwa dakika kumi kama mwili wako haujazoea kufanya mazoezi. Polepole, ongeza wakati huo uwe dakika mia na hamsini.
Mifano ya mazoezi hariri
umuhimu wa mazoezi hariri
Mazoezi yana umuhimu sana katika mwili wa binadamu kwa kuwa:
- mazoezi kama vile kunyanyua vyuma huimarisha mifupa na misuli
- mazoezi huboresha upatikanaji wa hewa na virutubishi kwenye seli za mwili
- mazoezi husaidia kuzuia maradhi na magonjwa kama vile saratani na pia usizeeke mapema
- mazoezi huboresha mfumo wa kupata usingizi
- mazoezi huongeza nguvu mwilini.
- Mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata maradhi makali kama vile shinikizo la damu, bolisukari
- Mazoezi huweza kupunguza uzani wa kupindukia kwa wale ambao wako katika hali hii.
Kwa sababu hizo tunashauriwa kufanya mazoezi ili miili yetu iwe imara na yenye afya nzuri. Tunashauriwa tufanye mazoezi kila asubuhi na mchana, kwa kunyoosha viungo kwa namna mbalimbali, ili kupunguza mawazo, na pia ili kuuweka mwili sawa, kuongezeka kwa ukuaji, kuzuia kuzeeka, kuimarisha misuli na mfumo wa moyo, kuvumilia ujuzi wa mashindano, kupoteza uzito, na pia kufurahia.
Kujilinda wakati wa mazoezi hariri
Tanbihi hariri
- ↑ Ritzmann, Ramona; Kramer, Andreas; Bernhardt, Sascha; Gollhofer, Albert (2014-02-26). "Whole Body Vibration Training - Improving Balance Control and Muscle Endurance" (in en). PLOS ONE 9 (2): e89905. . . . . http://journals.plos.org/plosone/article?id=10.1371/journal.pone.0089905.
- ↑ Laskowski, Edward R.. Is whole-body vibration an effective workout? (en-US). Iliwekwa mnamo 7 July 2018.
- ↑ Sudeshna Dey. KnockYourVibe: Frequency of vibration machines and its impact on the human body (en-US). KnockYourVibe - Learn about Whole Body Vibration Machines. Iliwekwa mnamo 7 July 2018.
Marejeo hariri
Viungo vya nje hariri
- https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/fitness/in-depth/exercise/art-20048389
- https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/physical-activity-its-important
- http://msthe.go.tz/health/battle-ropes-workout-routine-example/ Archived 15 Oktoba 2018 at the Wayback Machine.
- https://www.healthline.com/nutrition/10-benefits-of-exercise
- https://medlineplus.gov/magazine/issues/spring12/articles/spring12pg6-7.html
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mazoezi ya mwili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |