Mbuyu wa Ombalantu
Mbuyu wa Ombalantu (pia unajulikana kama Omukwa waaMbalantu, yaani Mti wa Uzima) ni aina ya mti mkubwa wa mbuyu unaopatikana mjini Outapi kaskazini mashariki mwa nchi ya Namibia katika barabara kuu ya Tsandi.
Ni mti wenye ukubwa wa mita 28 na futi 92 ukiwa na zaidi ya miaka 800.[1]
Ndani ya shina la mbuyu huo wanaweza kuingia watu 35. Ni mbuyu ambao uliwahi kutumika kama kanisa, kituo cha polisi, nyumba na sehemu ya kujificha katika matukio tofautitofauti kulingana na historia ya Namibia.
Kwa sasa ni kivutio na tangu mwaka 2004 mbuyu huo umekuwa ukitambulika kama sehemu ya urithi[2]
Sehemu za mbuyu huo zinaelezea kuhusu jamii ya Waovambo na pia historia ya mapambano ya uhuru wa Namibia [3]
Marejeo
hariri- ↑ Bause, Tanja. "Namibia: History of the Ombalantu Baobab Tree", 31 August 2010.
- ↑ Amukwaya, Yvonne. "The Baoba tree, Outapi's gold mine", Focus on the North supplement, page 7, 21 August 2014.
- ↑ "North (Omusati): Ombalantu Baobab Tree Heritage Centre and Campsite". Namibia Travel Online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Mei 2011. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2011.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbuyu wa Ombalantu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |