Mdhamini ni riwaya ya kipepelezi iliyoandikwa na Japhet Nyang'oro Sudi mwaka 2019 ikizungumzia kisa cha watoto watano waliopewa mafunzo mazito na kuhitimu kwa kiwango cha juu hadi kuiogopesha idara ya usalama wa taifa [1].

Watoto hao pacha wanakusudiwa kuingiza katika idara ya usalama wa taifa tayari wakiwa na kiwango cha juu cha mafunzo lakini muda mfupi kabla hawajatimiza lengo mpelelezi mahari na mhusika mkuu katika riwaya hii, Jacob Matata, anashutukia mchezo huo baada ya kupewa kazi na mkuu wake wa kitengo Bi Anita afuatilie sakata la watoto waliopotea miaka mingi iliyopita wakiwa hospitali tofautitofauti na kuwaacha pacha wenzao.

Kwa umahiri mkubwa, huku akishirikiana na baadhi ya majasusi wenzake na polisi, Jacob Matata anafanikiwa kuzima ndoto za mtu aitwaye Mdhamini aliejitolea kuwandaa watoto hao waliotishia usalama wa taifa.

Tanbihi hariri

  1. "MDHAMINI Page". somariwaya.co.tz. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-08. Iliwekwa mnamo 2020-02-07. 
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdhamini kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.